July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vitambulisho vya taifa kutafuna bil 160

Wananchi wa Morogoro wakijiandikisha ili kupata Vitambulisho vya Taifa

Spread the love

JUMLA ya Sh. Bilioni 160 zimetengwa kwa ajili ya mradi vitambulisho vya Taifa nchini. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Aidha, hadi Machi mwaka huu Sh. 56.8 bilioni zilikwishatolewa huku kiasi kilichobaki kinaendelea kutolewa na serikali kwa kadri hali ya fedha inavyoruhusu.

Kauli hiyo ilitolewa leo  bungeni na Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira  Silima alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mtambile, Masoud Abdallah Salim (CUF).

Mbunge huyo alitaka kujua kwa nini serikali inasuasua katika kuwawezesha NIDA kukamilisha zoezi la utoaji wa vitambulisho vya uraia.

Akijibu swali hilo, Silima amesema katika mwaka wa fedha 2014/15 ilitenga kiasi cha Sh. bilioni 160 kwa ajili ya mradi huo na hadi Machi, mwaka huu ilitoa Sh. Bilioni 56.8.

“Napenda kutoa taarifa kwa Bunge lako Tukufu kuwa utoaji wa Vitambulisho vya Taiga hivi sasa unaendelea vizuri kwani tayari Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa imekwishawatambua, kuwasajili na kuanza kutoa vitambulisho kwa wakazi wa Zanzibar, Dar es Salaam na Pwani,” amesema .

Amesema usajili unaendelea kwa wakazi mikoa ya Lindi, Mtwara, Morogoro na Tanga.

error: Content is protected !!