Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Vitambulisho vipya vya machinga 1 Aprili, Ma-RC, DC wapewa maagizo
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vitambulisho vipya vya machinga 1 Aprili, Ma-RC, DC wapewa maagizo

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema, vitambulisho vipya vya Wamachinga vilivyofanyiwa maboresho vikiwa na picha ya muhusika na baadhi ya kumbukumbu binafsi vitaanza vitaanza kutolewa tarehe 01 Aprili 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Amewataka, Wakuu wa Mikoa (RC) na Wilaya (DC), wahakikishe Wamachinga wanaendelea kufanya shughuli zao bila ya bugudha katika kipindi hiki ambacho muda wa matumizi ya vitambulisho vyao umekwisha.

Majaliwa amesema hayo jana jioni Alhamisi tarehe 28 Januari 2021, wakati alipofunga mkutano na viongozi wa Wamachinga kutoka mikoa yote Tanzania Bara, viongozi wa mabenki na baadhi ya mawaziri na watendaji wa Serikali katika Kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam

Alisema vitambulisho hivyo vipya, vilivyofanyiwa maboresho vitakuwa na picha ya muhusika na baadhi ya kumbukumbu binafsi zitakazomtambulisha na kumwezesha kupewa huduma katika maeneo mbalimbali zikiwemo na taasisi za kifedha.

Majaliwa alisema, vitambulisho hivyo vitakuwa na picha ya mhusika, hivyo haitawezekana kutumiwa na mtu mwingine na pia vitadumu kwa miaka miwili hadi mitatu tofauti na vya sasa ambavyo vilikuwa vya mwaka mmoja.

“Serikali kupitia John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeamua kutoa vitambulisho rasmi ambayo vitawatambulisha popote na kupata huduma muhimu kama vile kutambulika na taasisi za fedha na maeneo muhimu,” alisema

Kadhalika, Majaliwa aliwaagiza viongozi wa Wamachinga wahakikishe wanakuwa na takwimu sahihi idadi ya Wamachinga ili iwe rahisi kuwahudumia.

“Tuwe na kanzidata ya Wamachinga itarahisisha mawasiliano ndani ya Shirikisho la Wamachinga na Serikali,” alisema Majaliwa

Waziri Mkuu alisema, Wamachinga wajiunge pamoja kuanzia ngazi ya Vitongoji hadi Taifa ili waweze kuhudumiwa kwa urahisi.

“Mkijiunga pamoja na kutambuliwa ni rahisi kwa taasisi za kifedha kuwafikia na kuwapatia huduma za mikopo itakayowawezesha kukuza mitaji yenu.”

Alisema Serikali imedhamiria kumhudumia na kumtumikia kila mwananchi wakiwemo Wamachinga kwa lengo la kuwawezesha kukuza biashara zao na kujikwamua kiuchumi, hivyo aliwataka wafanye kazi kwa bidii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania yakabidhi rasmi msaada nchini Malawi

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari Mchanganyiko

Bashe: Tumeshagawa pikipiki 5,500 kati ya 7,000 kwa maafisa ugani

Spread the love  WAZIRI wa Kilimo, Hussen Bashe, amesema wizara hiyo tayari...

Habari Mchanganyiko

Spika Tulia awapa neno mawaziri utekelezaji mashamba ya pamoja

Spread the love  SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amewataka mawaziri kushirikiana...

error: Content is protected !!