Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Vita ya ruzuku CUF yatinga Mahakama ya Rufaa
Habari za SiasaTangulizi

Vita ya ruzuku CUF yatinga Mahakama ya Rufaa

Spread the love

BODI ya Wadhamini ya CUF imefungua shauri Na. 343/01/2018 katika Mahakama ya Rufaa, kupinga amri ya zuio la kutolewa ruzuku ya chama hicho iliyotolewa na Mahakama Kuu. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Bodi hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, iliwakilishwa na Peter Malebo, Thomas Malima na wengine 7, ambapo leo tarehe Mosi Novemba 2018, shauri hilo lilisikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Mussa Kipenka, Jaji Richard Mziray na Jaji Gerald Ndika.

Jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa itatoa hukumu juu ya hoja za awali za mapingamizi baada ya kutoa taarifa (NOTICE) kama ulivyo utaratibu wake. Na kwamba, kwa mujibu wa kanuni za Mahakama ya Rufaa hukumu inatarajiwa kutolewa ndani ya siku 14 kuanzia tarehe shauri liliposikilizwa.

Katika maombi yake ya msingi, bodi hiyo inaiomba mahakama ya rufaa kutengua uamuzi katika shauri Na. 80/2017 lililofunguliwa kwenye Mahakama Kuu Oktoba 2017, na Bodi ya Wadhamini inayomuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

Mahakama Kuu mbele ya Jaji Wilfred Dyansobera ilitoa amri ya kumzuia Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kutoa fedha za ruzuku ya CUF kwa Pro. Lipumba na wenzake, hadi pale maamuzi ya shauri Na. 21/2017 dhidi yake na Mwanasheria Mkuu wa Serikari (CAG) kuhusu tuhuma za kutoa fedha za ruzuku Sh. 369 milioni, yatakapotolewa.

Kesi hiyo ilifunguliwa na Bodi ya Wadhamini ya CUF inayomuunga mkono Maalim Seif, ikidai kuwa fedha hizo hazijulikani matumizi yake, pamoja na kutokuwa kwenye mikono salama kutokana kwamba Prof. Lipumba ambaye bodi yake ilikabidhiwa fedha hizo, alivuliwa uanachama.

Mvutano wa bodi hizo mbili ulikuja baada ya uwepo wa mgogoro wa kiungozi uliokikumba chama hicho, ambapo upande wa Maalim Seif unadai kuwa Prof. Lipumba si mwenyekiti halali kufuatia kuvuliwa uanachama wa CUF, wakati Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) ikimtambua kuwa kiongozi halali pamoja na bodi yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya...

BiasharaTangulizi

TLS wajitosa sakata la ukodishaji wa bandari

Spread the love  CHAMA cha wanasheria Tanzania (TLS), kimejitosa katika sakata la...

BiasharaTangulizi

Ngoma bado mbichi mkataba wa Bandari

Spread the love  SAKATA la mkataba wa uendeshaji, uendelezaji na uboreshaji wa...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mkataba unaweza kuvunjwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

error: Content is protected !!