Sunday , 25 February 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Vita vyapoteza watu 40 nchini Sudan
Kimataifa

Vita vyapoteza watu 40 nchini Sudan

Spread the love

WATU 40 wameuawa na kujeruhiwa katika mapigano mapya yaliyotokea katika jimbo la Yei nchini Sudan Kusini, anaandika Hellen Sisya.

Mapigano hayo ambayo yanatokana na mgogoro wa kisiasa nchini humo, yametokea kati ya jeshi la nchi hiyo pamoja na waasi wa taifa hilo.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mpaka sasa  watu wengi wameuawa na kujeruhiwa  katika vita vinavyoendelea nchini humo na umezitaka pande kuu hasimu katika mgogoro huo  kufanya juhudi za kurejesha amani na maridhiano.

Sudan Kusini ilitumbukia katika machafuko na mapigano kati ya wafuasi wa Rais Salva Kiir na makamu wake wa zamani Riek Machar tangu mwaka 2013.

Salva Kiir alimtuhumu makamu wake huyo kwamba alipanga njama za kufanya mapinduzi.

Baada ya kushamiri kwa mgogoro huo na kwa juhudi mbalimbali za  kimataifa mwaka 2015 pande hizo mbili zilifikia makubaliano ya kugawana madaraka.

Hata hivyo, kukiukwa kwa vipengele vya makubaliano hayo, kulipelekea kuvunjika kwa makubaliano hayo na kwa mara nyingine nchi hiyo changa zaidi barani Afrika ikatumbukia katika vita na machafuko.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

Kimataifa

Jeshi Kongo lazima jaribio la M23

Spread the loveJeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana Jumatano lilizima...

KimataifaTangulizi

Rais wa Namibia amefariki dunia

Spread the loveHAGE Gengob, Rais wa Namibia, amefariki dunia wakati akipokea matibabu...

error: Content is protected !!