July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vita Urusi-Ukraine: Tanzania yatangaza neema bei ya mafuta

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imetangaza kuondoa tozo ya Sh.100 kwa lita ya mafuta ya Dizeli, Taa na Petroli zinazopaswa kulipwa na watumiaji wa mafuta kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia tarehe 2 Machi hadi Mei 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Uamuzi huo umetangazwa leo Jumatatu tarehe 28 Februari 2022 na Wizara ya Nishati kutokana na kupanda kwa bidhaa hizo katika soko la dunia kutokana na mbalimbali ikiwemo vita vya Urusi na Ukraine.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba, Serikali itaendelea kutathimini mwenendo wa bei za mafuta katika soko la dunia.

 

“Pamoja na kwamba, uamuzi huu utaipunguzia Serikali mapato ya Sh.30 bilioni kwa mwezi, Serikali imeona ni muhimu kuwalinda wananchi wake dhidi ya athari za mabadiliko ya bei za mafuta ulimwenguni,” imeeleza taarifa hiyo

Katika taarifa hiyo, imefafanua kwamba, Waziri wa Nishati, January Makamba ameidhinisha na kusaini marekebisho ya kanuni inayohusika na tozo hiyo ili kutimiza uamuzi huo wa Serikali.

error: Content is protected !!