January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vita kinara wa mabao Ligi Kuu

Spread the love

 

WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara ikiendelea kupamba moto, kwa kupigwa michezo 11 kwa baadhi ya timu, vita nyingine imeibuka katika kutafuta mfungaji bora wa msimu huu 2021/22, mara baada ya wachezaji tisa kuonekana kubanana katika orodha hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Licha ya wachezaji hao tisa kubanana, lakini bado kumeoneka kuwa na ukame wa mabao kwa washambuliaji kwenye uwezo wa kupachika mabao mengi.

Katika orodha hiyo wachezaji watatu wamefungana wakiwa na mabao matano ambao ni Vitalisy Mayanga kutoka klabu ya Polisi Tanzania, George Mpole wa Geita Gold na Jeremiah Juma ambaye anakipiga kwenye klabu ya Tanzania Prisons.

Wachezaji sita waliosalia wote wamefungana wakiwa na mabao manne, ambapo kwenye orodha hiyo wapo Feisal Salum na Fiston Mayele wote kutoka Yanga, huku wengine ni Richardson Ng’ondya, Juma Luizio wote wa Mbeya City.

Pia kwenye orodha hiyo yupo Medie Kagere kutoka klabu ya simba ambaye alishawahi kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi cha miaka miwili, huku Relient Lusajo kutoka Namungo akifunga dimba hilo.

Ikumbukwe mpaka sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imebakisha michezo minne hadi mitano ili kukamilisha mzunguko wa kwanza.

error: Content is protected !!