June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vita dhidi ya Covid-19: Serikali yawaangukia viongozi wa kisiasa, kidini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi (katikati)

Spread the love

 

SERIKALI imewaomba viongozi wa dini na wa vyama vya siasa, wawe mstari wa mbele katika kuwahimiza wananchi kufuata miongozo ya kujikinga na maambuziki ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (Covid-19). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumatatu, tarehe 5 Julai 2021 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi, katika mahojiano yake na Kituo cha Televisheni cha Azam, jijini Dodoma.

“Ningependa kuomba sana viongozi wenyewe ndani ya Serikali, vyama vya siasa, dini na sekta binafsi, tuoneshe mfano kwa wananchi kwa kuchukua tahadhari dhidi ya Covid-19. Zingatieni kunawa maji katika ofisi zenu, tunawe mikono na kuvaa barakoa,” amesema Prof. Makubi.

Katibu mkuu huyo wa Wizara ya Afya, amesema viongozi hao wakifuata miongozo inayotolewa na wataalamu wa afya, dhidi ya kujikinga na Covid-19, wananchi watafuata nyayo zao. “tuepuke misongamano, sisi viongozi kama tukifanya hivyo, wananchi wataitikia vizuri.”

Prof. Makubi ametoa wito huo baada ya kuulizwa Serikali ina mpango gani, katika kuhakikisha wananchi wanafuata miongozo inayotolewa na wataalamu wa afya dhidi ya janga hilo.

Baada ya kubainika baadhi ya wananchi hawafuati miongozo hiyo, ikiwemo kuvaa barakoa, kukwepa mikusanyiko na kunawa mikono kwa maji tiririka.

“Kweli kuna baadhi ya changamoto ya watu kutofuata miongozo, nadhani wananchi ni waelewa na wako tayari. Sioni kama wana shida yoyote ni kuwaelimisha tu ili kujikinga na kuwakinga wengine,” amesema Prof. Makubi.

error: Content is protected !!