April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Visa vipya 14 vya Corona vyaripotiwa Tanzania

Spread the love

SERIKALI imetangaza ongezeko la  “kesi mpya kumi na nne” (14) za maambukizi ya ugonjwa wa Corona (Covid 19) nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaaam … (endelea).

Taarifa ya wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, iliyosainiwa na waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu, imeeleza kuwa wagonjwa wote wapya, ni Watanzania.

“Wizara inatoa taarifa kuwa kuna ongezeko la wagonjwa wapya 14 kutoka 32 waliokuwapo awali,” ameeleza Waziri Ummy na kuongeza, “kati ya hawa wagonjwa 13 wamepatikana Dar es Salaam na mmoja jijini Arusha.”

Amedai kuwa wagonjwa wote hao wanaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa wataalam wa afya.

Amesema, serikali inaendelea kufuatilia watu waliokaribu na wagonjwa hao na kwamba serikali inaendelea kuwataka wananchi kuepuka misongamano.

Hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuripoti idadi kubwa ya wagonjwa wa Corona kwa mara moja, tangu kuibuka kwa ugonjwa huo takribani mwezi mmoja uliyopita.

error: Content is protected !!