Wednesday , 21 February 2024
Home Kitengo Maisha Afya Virusi vya Corona: Tahadhari ya Rais Magufuli kwa taifa
AfyaHabari za Siasa

Virusi vya Corona: Tahadhari ya Rais Magufuli kwa taifa

Spread the love

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kuchukua tahadhari kutokana na kusambaa kwa virusi vya Corona. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Karakana Kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), leo tarehe 14 Machi 2020 amesema, ugonjwa huo upo, na iwapo kila Mtanzania hatochukua tahadhari yeye na watu wanaomzunguka, ‘tutakwisha.’

“Kila mmoja kwenye familia zetu tutoe tahadhari ya hali ya ugonjwa wa Corona, iwe shuleni, vyuo, makambini na kwenye magari iwe kabla hupanda kwenye dalalala, kondakta atoe elimu kidogo.

“Ndugu zangu waandishi wa habari, ikiwezekana kila siku tutoe ujumbe wa ugonjwa wa Corona, angalau hata kwa maneno matatu. Kwenye TV zetu, kwenye redio zetu, kabla hata hujatangaza taarifa ya habari, pawepo hata mistari miwili ya maneno ya kupambana na Corona, tukidharau ndugu zangu tutakwisha,” amesema Rais Magufuli.

Amesema, tayari nchi nyingi zimetoa tahadhari ikiwa ni pamoja na kuzuia ndege zao kwenda huo, zimeopunguza safari, “ndege yetu iliyoenda India jana, ikirudi leo haitaenda tena.”

“Tuchukue tahadhari, tusipeane mikono, tusibusuane, sifahamu usiku watafanyake, lakini napo unaweza kukwepa usibusu mambo yakawezekana na miraha ikaendelea,’” amesema.

Amesema, anawaomba viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali kuliombea taifa kwa kila mtuna na imani yake huku akisisitiza kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuendelee kusimamia mipaka ya nchi, ili kila anayeingia awe ameangaliwa.

“Tunatambua kuwa Tanzania hatujapata mtu wa ugonjwa huo mpaka sasa, lakini Tanzania hatuwezi tukajiweka pembeni bila kuchukua hatua,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!