May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vipimo vya corona vyachelewesha mchezo Namungo Vs Nkana

Spread the love

 

MCHEZO wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Namungo FC ya Dar es Salaam, Tanzania na Nkana ya Zambia, umechelewa kuanza kwa dakika 60. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ni baada ya wachezaji wa Nkana, kugomea kupimwa vipimo vya maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19).

Ili kujikinga na maambukizi kwenye michezo ya Kombi la Shirikisho na ile ya Klabu Bingwa Afrika, Shirikisho la Sola Afrika (CAF), limeweka utaratibu wa kupimwa COVID-19, kabla ya mchezo.

Mchezo huo, ulikuwa uanze saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam leo Jumapili tarehe 4 Aprili 2021, umejikuta ukianza saa 11:00 jioni.

Timu zote mbili, zilitumia takribani dakika nane kupasha misuli kuanzia saa 10:38 hadi saa 10:44 jioni, zikarejea vyumbani kujiandaa kwa mchezo huo wa kundi D.

Haijafahamika haraka makubaliano yaliyofikiwa, hadi kuruhusu mchezo huo kuchezwa pasina timu ya Nkana kupimwa COVID-19.

Timu zingine kwenye kundi hilo ni Pyramid ya Misiri inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi sita sawa na Raja Casablanca ya Morocco lakini zikiwa na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Namungo na Nkana zote hazina pointi yoyote.

error: Content is protected !!