October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vipaji vya watoto kusakwa Leaders Club

Spread the love

KAMPUNI ya kuandaa filamu nchini Tanzania (J FILM 4 LIFE), imeanza utaratibu wa kutafuta vipaji vya kuigiza kwa watoto ili kushiriki kwenye vilamu mpya ya watoto wanayotarajia kuiandaa. Anaripoti Martin Kamote….(enedelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 2 Septemba 2019, mmiliki wa kamopuni hiyo, Jenifer Kyaka ambaye ni maarufu kwa jina la Odama amesema, kampuni hiyo mpaka sasa imeweza kutengeneza filamu zaidi ya 21  na tanthilia.

“Leo ni siku muhimu sana katika sekta ya tasnia yetu ya filamu hasa kwa watoto hapa nchini Tanzania kwasababu, nazindua rasmi mchakato wenye lengo la kutafuta na kuvumbua watoto wenye vipaji vya kuigiza katika tamthilia.

“Watakaochaguliwa, nitawashirikisha katika tamthilia mpya ya watoto inayokuja kuandaliwa na kampuni,” amesema.

Pia amesema, pamoja na ukuaji wa tasnia ya filamu nchini, pia kumekua na changamoto mbalimbali katika soko na tasnia kwa ujumla wake.

Na kwamba, miongoni mwa changamoto ni kutokuwepo kwa mifumo na njia za uhakika katika uuzaji na usambazaji wa filamu, hivyo kupelekea soko kuanza kuhama kutoka katika filamu kuelekea kwenye tamthilia.

https://youtu.be/Q3G_Q8hpq90

Amesema, JFILM 4 LIFE imeamua kuanza mchakato wa  kuandaa tamthiliya kubwa inayolenga watoto, ikielezea zaidi maisha yao katika mambo mbalimbali.

“Miongoni mwa mambo katika tamthilia hiyo ni pamoja na elimu, afya,  migogoro ya familia kwa watoto, dini, mirathi, tamaduni na mila,unyanyasaji wa watoto na ubakwaji,” amesema.

Kazi ya kupata watoto wenye vipaji  vya kuigiza itafanyika Jumamosi tarehe 14/09/2019 saa 3 kamili asubuhi katika viwanja vya Leaders Club kuanzia saa tatu kamili asubuhi.

error: Content is protected !!