December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Viongozi watakiwa kutoingiza siasa katika utunzaji wa misitu

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja

Spread the love

 

VIONGOZI nchini wametakiwa kuacha kufanya siasa kwenye ardhi bali waitumie katika kuboresha shughuli za usimamizi endelevu wa misitu ikiwemo kuweka mipaka ya asili na kuondoa migogoro baina ya vijiji hasa katika maeneo yasiyowekewa mipango ya matumizi bora ya ardhi. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja alisema hayo jana kwenye Mkutano mkuu wa 22 wa Mtandao wa jamii wa usimamizi misitu Tanzania (MJUMITA) uliofanyika mjini hapa ambapo alisema binadamu wanaongezeka kila siku lakini ardhi haiongezeki hivyo isifanywe siasa kwenye ardhi itaharibu usimamizi wa misitu jambo ambalo hata vitabu vya dini vinakataza na ardhi inaweza kukuhukumu.

Masanja alisema ni wakati sasa umefika kwa watendaji na wenyeviti wa vijiji kusimamia vyema misitu iliyopo na kutoigawa kiholela bali waendeshe uvunaji endelevu wa misitu pale inapobidi ambao hautaathiri misitu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

“nashukuru katika kikao hiki hata madiwani mpo, mkasimamie masuala ya usimamizi wa misitu ya vijiji na kata zenu, tusifanye siasa kwenye ardhi, itatuhukumu” alisema.

Alisema uharibu wa misitu unaweza kuleta athari kubwa kwa jamii nan chi kwa ujumla ikiwa ni pampja na kuharibu vyanzo vya maji, kuharibu rutuba ya udongo, kuharibu ikolojia ya viumbe hai na mwisho wa siku kuchangia katika mabadiliko ya tabianchi.

Hata hivyo aliitaka MJUMITA kutoa elimu kwa wakazi wa kanda ya Ziwa ambao mpaka sasa bado hawajapata elimu ya utunzaji mazingira ili kusaidia kupunguza au kuondoa ugpotevu wa misitu wanaofanya pale wanapopata eneo la makazi mara wanapoomba kutoka kwa wenyeviti wa vijiji.

Alisema wafugaji wanapokaribishwa kwenye eneo wanakwenda wenyewe lakini wakishapewa ardhi bila uangalifu wanageuka kuwa mwiba mkali katika matumizi holela ya ardhi jambo ambalo linapaswa kubadilishwa.

“Kama hali ya sasa ya uharibifu wa misitu isipodhibitiwa, tujue miaka 10 ijayo hali itakuwa mbaya zaidi, Kizazi kijacho kutakuja kutulilia, sababu ya uwepo wa upotevu mkubwa wa misitu unaofanywa kwa sasa” alisema Naibu Waziri huyo.

Alisema takwimu zilizopo zinaonesha takribani hekta 460,000 za mistu, zaidi ya ukubwa jiji la Dar es Salaam hupotea kila mwaka kwa ajili ya shughuli za uharibifu wa misitu.

Masanja alisema kimsingi, misitu inaruhusiwa kuvunwa kwa njia endelevu baada ya wahusika kupata vibali, lakini kwa bahati mbaya uvunaji holela wa misitu kwa ajili ya mbao, kuni na mkaa ndio umekuwa ukifanyika zaidi nchini.

Alisema ni lazima matumizi bora ya ardhi katika kila kijiji yatiliwe mkazo hata kwa njia zisizo rasmi kwa kutenga eneo la malisho, vyanzo na maji na misitu kwa ajili ya kufugia nyuki au kilimo cha uyoga ili kuepukana na uharibifu wa misitu.

“akina mama wa vijijini wanatumia zaidi kuni ambazo kimsingi alisema ni matawi na hivyo kama kuna uharibifu wanafanya ni asilimia moja pekee, lakini wanaosababisha uharibifu mkubwa ni watu wa mijini wanaoendelea kutumia mkaa wakati wengi wao wanaweza kutumia nishati safi ya kupikia (gesi na umeme).

Naye Mkurugenzi wa MJUMITA, Rahima Njaidi, alisema malengo ya mkutano huo mkuu ni kujadili mafanikio na changamoto na kuja na maazimio ya pamoja kuhusu mikakati ya kuchukua katika kulinda misitu.

Alisema Mjumita ina wanachama takribani 15,000 wanaoishi kandokando ya misitu ya asili, katika mikoa 13, wilaya 30 na malengo ya shirika hilo lisilo la kiserikali ni kufanya uhifadhi endelevu wa misitu ya asili.

Naye Mwenyekiti wa MJUMITA Taifa, Rehema Ngelekele alitaja baadhi ya changamoto zinazoukabili mtandao huo kuwa ni uhaba wa raslimali fedha na baadhi ya vijiji kutopimwa na hivyo kutokuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi, baadhi ya wanachama kutegemea zaidi misitu kutokana na kukosa shughuli nyingine za kuwaingizia kipato na baadhi ya viongizi kutumia madaraka yao vibaya katika usimamizi wa misitu.

Naye Mlezi wa Mjumita, Charles Meshack alisema nchi inahitaji misitu pengine kuliko misitu inavyowahitaji watu ambapo spidi ya kupotea kwa misitu inapaswa kufanyiwa kazi vinginevyo baada ya miaka 20 nchi haitakuwa na msitu iliyobaki na watayoizungumzia.

error: Content is protected !!