June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Viongozi “wajifunga” kutunza amani

Viongozi wa Kisiasa na kidini wakiwa kwenye mkutano wa Amani na Utulivu ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere

Spread the love

MKUTANO wa kujadili amani na utulivu Tanazania umemalizika chini uongzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kuwashirikisha viongozi vya vyama vya siasa, wazee, viongozi wa dini na viongozi wastaafu wa serikali. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Mengi yamejadiliwa katima mkutano huo, ambapo msemaji wa taasisi ya Mwalimu Nyerere, Gertrude Mongella, amesema “Kazi hii ya kujadili amani na utulivu wa taifa letu imeandaliwa kwa kuzingatia dhamana tuliyopewa na kuachiwa na baba wetu wa taifa, katika kutekeleza mawazo yake, imani yake, mwelekeo wa nchi hii mpaka hapo ameifikisha ili tuweze kuendelea.”

Anasema kuwa, tasisi hii shabaha yake kubwa ni kuhakikisha kwamba Watanzania wana mahali pa kuzungumzia kwa uhuru, uwazi, umakini na upendo kuhusu masuala yanayohusu nchi yao. Kwamba hicho ndicho kimefanyika.

“Mawazo yaliyotolewa tutayafikisha kwa njia moja au nyingine kwa Watanzania na vyombo husika angalau kuzungumzia suala la amani bila kigugumizi,”amesema.

Akifungua mkutano huo, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema “Tumezitumia siku mbili hizi kujadili hali ya nchi yetu na kutafuta hatma yake. Tanzania ni nchi ambayo imejipambanua duaniani kote kwa umoja na amani kwa mshikamano.”

Ameongeza kuwa Tanzania ni mfano wa kuigwa kila uendaka duniani. “Kila mmoja angependa hali hiyo izidi kuimalika lakini ukweli ulio dhahili ni kwamba, kama tulivyosema sote kuna viashiria, kuna dalili kwamba haya ambayo tunajivunia yanaweza kuchafuka.”

Seif anasema kuwa, hayati Mwalimu Nyerere mara nyingi alisema kwamba “tusidhani yanayotokea kwingine, Tanzania hayawezi kutokea. Tuwe waangalifu.”

Ameshawishi kuwa, “kila mmoja aliyeshiriki hapa ameoneshwa kukerwa na hizi dalili ambazo zinaweza kuwa ni chanzo cha kuvurugika kwa amani. Tumetumia siku mbili hizi kutathmini hali ilivyo, na ni kwa nini tukafika hapa na kubwa zaidi tufanye nini kuidhibiti hii hali ili Tanzania ibaki ni nchi ya amani, umoja na usalama na msikilizano.”

Seif ameongeza kuwa, tamko leo limeeleza kwa ufupi kwamba itasaidia kujinusuru na balaa hili. “Ni matumaini yangu sisi tutakuwa mabolozi, vyombo vya habari vipo. Vitayapa uzito na kuyaandikia makala ili wananchi wazidi kuyaelewa. Lakini na sisi pia tuna wajibu huko tunakotoka, haya tuliyozungumza na kukubaliana tutangaze kwa wenzetu.”

Mwakilishi wa viongozi wa dini, Tarasius Ngalalekumtwa, kutoka Baraza la Maaskofu (TEC), amesema, “Kumnyima binadamu haki zake, athari zake sio ndogo. Hakuna binadamu atakaekubali kukandamizwa.

“Amani ni tunda la malezi ya kiutu na kidini. Maana dini zote zinahubiri suala hili. Binadamu ameubwa ili afurahie zawadi ya amani. Kwa uhuru wenye uwajibikaji na hivyo, amani itapatikana tu pale penye haki na usawa kwa wote”.

Dk. Willibrod Slaa – Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa niaba ya vyama vya siasa, amesema “Amani ni tunda la haki, ukweli, uwazi; na taifa likijikita katika hayo, wote tutaishi katika amani”.

Amesema “nchi ni yetu. Taifa ni letu. Hatuna mahali pengine pa kwenda. Tutazikwa hapahapa wote. Iwe ni sisi, watoto wetu, wajukuu zetu na wote tunajua babu zetu wako hapa. Amani ikiharibika katika nchi sisi sote tumeharibika. Na mafunzo tunayo.

“Sasa hivi tunavyoongea nchi jirani ya Burundi, wananchi wamekimbilia kwetu. Ndani ya siku mbili kwa taarifa zilizopo watu wawili wamepoteza maisha. Sio tu kufikiria kukimbia hata usalama wa maisha siyo wa uhakikika”.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa wazee, Ahmada Hamis- mjumbe wa Baraza la Wazee kutoka Zanzibar, amesema “Taasisi ya Mwalimu Nyerere iliona mbali. Na wakaona mwelekeo unapotea.  Wakatuita sisi ili tuweze kujadili kwa kina suala hili”.

Amefafanua kuwa, kila mtu ana hamu na amani. Kwamba, kukaa na kushauriana ni jambo kubwa na hivyo kuahidi kupeleka ujumbe huo kwa wenzao.

error: Content is protected !!