Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Viongozi, wadau wa siasa waibua mambo 80, wato tamko tume huru, mikutano ya hadhara
Habari za SiasaTangulizi

Viongozi, wadau wa siasa waibua mambo 80, wato tamko tume huru, mikutano ya hadhara

Profesa Rwekaza Mukandala
Spread the love

OFISI ya Msajili wa vyama vya siasa pamoja na Baraza la Vyama vya Siasa limebebeshwa zigo la mambo 80 yaliyojadiliwa katika mkutano wa wadau wa siasa uliokuwa umelenga kujadili hali ya demokrasia ya vyama vya siasa nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Katika mkutano huo ulioanza juzi na kufikia tamati leo tarehe 17 Disemba, 2021 suala la mikutano ya hadhara, katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ndivyo vilivyotikisa huku viongozi na wadau wa siasa wakiacha jukumu hilo kwa Msajili wa vyama vya siasa kuunda kikosi kazi.

Kikosi kazi hicho kitakachoundwa na Msajili wa vyama vya siasa, kitatoa mapendekezo kwa baraza la vyama vya siasa ambalo litayapitisha na kuyapa uhalali na kuyafikisha kwa mamlaka husika.

Akisoma maazimio ya mkutano huo uliofungwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussen Ali Mwinyi, Mwenyekiti wa Mkutano huo, Profesa Rwekaza Mukandala amesema wanakongamano wameazimia kwamba badala ya kuendelea na mchakato wa katiba mpya, wanaweza kuchagua mambo machache yanayolalamikiwa sana na kuanza kuyafanyia kazi.

Pia kwa mujibu wa kifungu cha 11 cha sheria ya vyama vya siasa, vyama vya siasa ni haki yao kufanya mikutano ya kisiasa chamsingi kuwepo kwa utaratibu wa kuadhibiana pale au kwa vile ambavyo vinakiuka taratibu hizo.

Pia suala la mikutano ya hadhara, lishughulikiwe kwani hakuna haja ya kurudi mwanzo bali kinachotakiwa ni kurekebisha sheria ya katiba iliyopo sasa, katiba pendekezwa na kuipitisha.

Kuhusu masuala ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Prof. Mukandala amesema yamepokelewa na yanayohitaji kufanyiwa kazi, yatafanyiwa kazi.

“Wanakongamano wameazimia kwamba mkutano kama huu ni muhimu tudumishe utaratibu wa kukutana mara kwa mara ili kutatua changamoto kwa njia ya mazungumzo.

“Kwamba kuna umuhimu wa wadau wa siasa kufuata katiba, sheria, kanuni na miongozo katika kutekeleza majukumu yao pia vyombo vyenye maamuzi vina wajibu wa kutenda haki na kulinda amani kwani amani msingi wake ni haki.

“Kwamba vyama vya siasa vitoe nafasi maalumu kwa makundi maalumu husuani wanawake na wenye ulemamvu kwani michango yao ni muhumu kwa Taifa pia demokrasia inategemea na mazingira ya nchi husika, uchumi, mila, utamaduni na desturi za nchi husika hivyo tusiwe watu wa kuiga demokrasia ya nchi nyingine.

“Kwamba elimu ya uraia iwe endelevu, ianzie ngazi ya chekecheke isisubiri wakati wa uchaguzi na serikali na vyombo vya dola, viepuke upendeleo vinapohudumia vyama vya siasa na wananchi kwa ujumla,” amesema.

Ameongeza kuwa; Sheria ya vyama vya siasa ifanyiwe mapitio upya na mchakato uwe shirikishi pia sheria ya jeshi la polisi ifanyiwe mapitio yatakayofanya jeshi hilo kwa kisingizio cha kutekeleza sheria.

Pia viongozi wa siasa wawe hofu ya Mungu katika utendaji wa kazi zao kuwa waadilifu, watii sheria, wawe na uzalendo na kuwa na uchungu na nchi na kila moja ana jukumu la kulinda amani na utulivu ndani ya nchi  na kwamba kila mmoja anatembea katika jahazi moja likitobolewa watazama wote.

“Manung’uniko na malalamiko ya wananchi na wadau yashughulikiwe mapema tusisubiri shida zijitokeze pia Baraza la vyama vya kisiasa lipewe jukumu la kushughulikia migogoro ndani ya vyama vya siasa.

“Kama kuna malalamiko na kutoaminiana kwa wale wanaotuongoza hasa wale wanaoongoza tume zetu za uchaguzi, hata wakichaguliwa watu wengine, watu ndio sisi watanzania, hivyo tusipoaminiana maneno yataendelea kwa hiyo kuna haja ya kuongeza kuaminiana, wananchi, vyombo mbalimbali na viongozi wote,” amesema.

Aidha, akifunga mkutano huo Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali zote mbili zitayafanyia kazi mapendekezo hayo yaliyopitishwa na mkutano huo kwa masilahi mapana ya Taifa.

Pia amewasisitiza viongozi hao wa kisiasa pamoja na wadau wa siasa kuitunza na kudumisha amani kwani hata tafiti zinaonesha kuwa Tanzani ni miongoni mwa mataifa saba yenye kiwango kikubwa cha usalama na amani Barani Afrika.

Hata hivyo, amesema Baraza la Vyama vya Siasa lililoandaaa mkutano huo, limetokana na miafaka mitatu iliyofanyika kwa nyakati tofauti Visiwani Zanzibar pindi palipotokea sintofahamu katika chaguzi za Zanzibar.

Mkutano huo ulifunguliwa tarehe 15 Disemba, 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan umeshirikisha viongozi mbalimbali vya vyama vya siasa isipokuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na NCCR Mageuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

error: Content is protected !!