Tuesday , 3 October 2023
Home Habari Mchanganyiko Viongozi wa Serikali watua Morogoro kuweka mambo sawa ajali ya moto
Habari Mchanganyiko

Viongozi wa Serikali watua Morogoro kuweka mambo sawa ajali ya moto

Spread the love

BAADA ya vifo vya watu takribani 60 vilivyotokana na lori la mafuta kuwaka moto mkoani Morogoro viongozi mbalimbali wamewasili mkoani hapa kwa ajili ya kusimamia taratibu zote za kusafirisha mili na kusimamia huduma kwa majeruhi wa ajali hiyo. Anaripoti Hamisi Mguta, Morogoro … (endelea).

Moto huo uliozuka tarehe 10 Agosti 2019 ulisababisha vifo vya watu hao waliokuwa wakichota mafuta yalitomwagika kutoka katika lori hilo ambalo awali lilipata ajali na kupinduka baada ya dereva wa lori kupoteza muelekeo alipokuwa akimkwepa mwendesha pikipiki ndipo wananchi walipojitokeza wakiwa na ndoo na madumu kwa ajili ya kuchota mafuta yalikuwa yakimwagika.

Miongoni mwa viongozi waliowasili mkoani hapa ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Steven Kebwe.

Akizungumza nje ya hospitali ya rufaa ya mkoani wa Morogoro,  ambapo mili ya watu waliofariki ilipohifadhiwa wakiwemo pia na baadhi ya majeruhi, Kebwe amewaambia waandishi wa habari kuwa mara baada ya kupata taarifa za moto aliamuru umeme ukatwe na kuwataarifu watu wa zimamoto na uokoaji hivyo ilisaidia kupunguza kasi ya moto huo.

“Bila kufanya hivyo moto ungeweza kusambaa sana, tumefanya kazi kubwa na tulifanikiwa kuzima moto, majeruhi 68 waliungua vibaya sana na kati ya hao 39 walikuwa wameungua vibaya sana zaidi ya asilimia 50,” amesema.

Hata hivyo, Mhandisi Kamwelwe amesema serikali bado unaendelea kuweka utaratibu mzuri kwa ajili ya watu ambao wanahitaji kuitambua mili ya ndugu zao kwenda na kuangalia na kuhakiki kutokana na namna ilivyoungua haiwezi kutambulika haraka.

“Tunajua kuna watu ambao wapo nje ambao hawana uhakika kama wamepoteza ndugu tunaweka utaratibu ili tuweze kutambua miili hiyo na kufanya mazishi kwa mujibu wa mila na taratibu zetu,” amesema.

Naye Mhagama amesema kuwa wizara ya afya tayari imeshaleta madaktari bingwa kwa kazi ya kuhakikisha wanaokoa maisha ya majeruhi ambao wameungua vibaya na kuwa zimetengwa ndege mbili kwa ajili ya kusafirisha majeruhi ambao watahitaji matibabu zaidi nje ya mkoa huo.

“Katibu Mkuu wizara ya afya yupo hapa pamoja na MSD wapo kwa ajili ya kuhakikisha dawa zinapatikana na mambo ya ndani tumewapa kazi ya kuunda kamati maalum kuona ni namna gani tunaweza kuchukua vinasaba kwa ajili ya kuwatambua,” amesema.

Hadi sasa jumla ya watu walioripotiwa kufariki ni 64 miongoni mwao wakiwemo wanawake 24 ambapo pia awali kabla ya moto huo kuzuka takribani lita 60 za mafuta ya petroli zilipotiwa kukamatwa kutoka kwa waliokuwa wakisomba mafuta hayo kutoka kwenye lori na yaliyomwagika chini.

Hata hivyo dereva na kondakta wa lori hilo wameripotiwa kufariki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wawili wanaswa wakitengeneza noti bandia

Spread the loveJESHI la Polisi mkoani Songwe limewakamata watu wawili kwa tuhuza...

AfyaHabari Mchanganyiko

Chanjo mpya ya malaria Sh 5,000-10,000

Spread the loveShirika la afya la Duniani (WHO) limeridhia chanjo ya pili...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wagonjwa kiharusi waongezeka, Hospitali Mkapa yaja matibabu mapya

Spread the loveHOSPITALI ya Benjamini Mkapa kwa kushirikiana na madaktari Bingwa kutoka...

Habari Mchanganyiko

Wananchi waamua kujenga zahanati kukwepa adha kufuata huduma mbali

Spread the loveWANANCHI wa Kijiji cha Kwikerege, kilichopo katika Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!