Tuesday , 16 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Viongozi wa Dini wazindua Kitabu cha Mwongozo wa Uchumi
Habari Mchanganyiko

Viongozi wa Dini wazindua Kitabu cha Mwongozo wa Uchumi

Viongozi wa TEF na Bakwata wakizindua kitabu
Spread the love

KAMATI ya Viongozi wa Dini ya Masuala ya Haki za Kiuchumi na Uadilifu katika Uumbaji (ISCEJIC), imezindua Mfumo wa Soko Jamii unaotoa muongozo juu ya namna taifa litafikia kwenye uchumi imara unaogusa maisha ya Watanzania wote. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Mfumo huo umezinduliwa leo tarehe 12 Julai 2019 jijini Dar es Salaam, chini ya kamati ya ISCEJIC inayoundwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

Akielezea kwa ufupi kuhusu mfumo huo Ponsian Ntui,  mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine cha Jijini Mwanza (SAUT) amesema, mfumo wa uchumi wa soko jamii umejumuisha mifumo ya uchumi wa ujamaa na ubepari, ambao binadamu ndio kiini na mwenye maamuzi ya shughuli zote za kiuchumi.

Ntui amesema, mfumo huo unajumuisha ukuaji wa uchumi endelevu na ushirikishwaji ili kuleta maendeleo kwa watu wote, ambao umependekeza aina ya uchumi wa soko unaolinda na kudhibiti shughuli zote za uchumi.

“Rais John Magufuli alisema, anatamani aache mabilioni 100 lakini watapatikanaje. Alisema, tuna nchi kubwa watu wachache wanalipa kodi lakini ujiulize, ili walipa kodi wawe wengi unatakiwa ufanye nini?

“Alisema, makusanyo ya kodi ni madogo haridhiki, lakini unatakiwa kufanyaje? majibu ya haraka ni mfumo wa leo,” amesema Ntui.

Amesema, mfumo wa uchumi wa soko jamii una majibu juu ya changamoto ya ukosefu wa ajira, huduma za kijamii na kadhalika.

“Ukitaka kuondokana na tatizo la ajira, linda anachogundua mtu, lazima kila mtu alindwe kwa kile anachokipata, lazima tuwe na mfumo unaotabirika.  Uchumi wa soko jamii huu unasisitiza kwenye mfumo unaotabirika,” amesema na kuongeza Ntui.

“Tukaona njia pekee ni huu uchumi.Tukiutumia huu mfumo ambao unamwangalia binadamu kama msingi wa maamuzi tutatoka pale.Watu wetu wasifundishwe kwenye chuo tuu bali  waunganishwe kwenye soko pia.”

Askofu Steven Munga, Mwenyekiti wa ISCEJIC amesema, mfumo huo ni tunda la utafiti wa viongozi wa dini mbalimbali nchini, wakishirikiana na timu ya wataalamu wa ndani na nje ya nchi katika mambo ya uchumi wa soko jamii.

Askofu Munga amesema, mfumo huo una majibu ya changamoto za masuala ya maendeleo ya wananchi, biashara na uchumi.

 Ameiomba serikali, wasomi, sekta binafsi na Watanzania kwa ujumla, kuufanyia kazi mfumo huo, kwa minajili ya kuleta fursa ya kuibadilisha Tanzania kuwa nchi yenye uchumi imara, shirikishi na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Katibu wa TEC Padri Charles Kitima ambaye ni Mratibu wa mfumo huo, amesema mfumo huo umeanisha masuala manne ambayo kama serikali na wadau wengine watayafanyia kazi, yatasaidia kuimarisha uchumi wa kijamii.

Padri Kitima ametaja masuala hayo, ikiwemo utawala mzuri serikali katika kusimamia muenendo wa shughuli za kiuchumi. Jumuiya ya Wafanyabiashara na elimu.

Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke amesema uzinduzi wa mfumo huo ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya viongozi wa dini katika kuhakikisha kwamba waumini wake wanapa maendeleo.

“Viongozi wa dini tuna wajibu mkubwa kusimamia amani ya nchi, sababu hatuwezi kuwa na amani kama watu wamekata tamaa. Napenda kutoa wito kwa viongozi wa dini, kuhamasisha watu kutumia mfumo huu,” amesema Sheikh Kabeke.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Sekta binafsi yasifu utekelezaji wa Mkumbi

Spread the loveSERIKAL imepongezwa kwa utekelezaji wa mapendekezo ya sekta binafsi kupitia...

Habari Mchanganyiko

Kamati ya bunge yapigia chapuo kilimo ikolojia

Spread the loveSERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imeshauriwa kushirikiana na wadau wa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yapata hasara 113 milioni hospitali kuwapa misamaha wagonjwa wasiostahili

Spread the loveSERIKALI imepata hasara ya kiasi cha Sh. 111.76 milioni, baada...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

error: Content is protected !!