July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Viongozi wa dini wawaasa Watanzania

Spread the love

VIONGOZI wa dini mkoa wa Dodoma wamewataka watanzania kuachana na mihemko ya kisiasa na badala yake wanatakiwa kuwa makini ili kuhakikisha wananchagua kiongozi makini mwenye kujua shida za watu. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Ushauri huo ulitolewa jana na Askofu wa kanisa la Methodist Jimbo la Dodoma, Joseph Bundara alipokuwa akizungumza na Mwanahalisi Online juu ya mwenendo wa kisiasa nchini.

Amesema ili kupata kiongozi ambaye ni mwadilifu na mwaminifu ni wajibu wa wananchi kuhakikisha wanamchagua kiongozi ambaye ana nia ya kuwakomboa watanzania ambao wanakabiliwa na dimbwi la umasikini.

Askofu huyo alisema kwa sasa kuna vijana wengi ambao wanafanya ushabiki wa kisiasa bila kuwa na fikra ya kumchagua kiongozi ambaye anaweza kuondoa tatizo la watanzania.

Wakati huo huo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Biblia kinachomilikiwa na Kanisa la Tanzania Assembless of God Tanzania, Jonas Mkoba amesema kwa sasa Tanzania inatakiwa kukubali mageuzi ambayo yanalenga kuwaondoa watanzania katika umasikini.

Mbali na mambo mengine ni wakati wa watanzania kuhakikisha wanafanya maombi ya kutosha kwa ajili ya kupata kiongozi ambaye anaweza nguvu ya mungu.

Mkuu huyo wa amesema watanzania wana haki ya kuwatambua viongozi ambao wana dhamira ya kweli katika kuwapatia maendeleo watanzania na si vinginevyo.

Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Mungu Tanzania, Sebastian Mcheri amesema kampeni na uchaguzi ni vizuri zikafanyika kwa amani na kuepuka maneno ya kudhalilishana na kutukanana.

“Sisi watumishi wa Mungu kwa imani zetu tunatakiwa kujitoa na kuliombea taifa ili kampeni na uchaguzi ziende kwa amani,” anasema.

error: Content is protected !!