May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Viongozi wa dini wapewa ujumbe

Spread the love

 

WATUMISHI wa Mungu, wameitwa duniani siyo kubomoa bali wanatakiwa kujenga ili watu waweze kumcha Mungu na kuachana na maovu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchungaji wa Kanisa la Maisha ya Ushindi lililopo eneo la Kigogo Freshi, Nelius Celemence amesema hayo hivi karibuni, alipokuwa kwenye ibada.

Amesema, mtumishi wa Mungu unapoanza kutoa maneno mabaya yanasababisha waumini kujigawa matokeo yake anabomoa badala ya kujenga.

Celemence alisema, kanisa la leo linahitaji maadili mema hasa kwa vijana, kina baba na mama ambao wanatakiwa kulifuata neno la Mungu litakalowasaidia kuondokana na matendo maovu ambayo hayampendezi Mungu.

“Kanisa la sasa linahitaji maneno mazuri na ya baraka na siyo maneno mabaya ya kuwasema watu na kuwakashifu na kuliponda neno la Mungu,”alisema Celemence.

Pia, aliwataka waumini kutafakari sheria za Mungu ambapo alitolea mfano kitabu cha Zabuni 1:1 hadi wa 6, Daudi anazungumzia kuhusu kukaa mbele ya mwenye mizaha.

Alisema mizaha inaondoa uwepo wa Mungu mfano mtumishi anapokaa.

error: Content is protected !!