VIONGOZI wa dini nchini Tanzania, wamemwomba Rais wa Taifa hilo, Samia Suluhu Hassan kutumia mamlaka aliyonayo kumaliza kesi ya ugaidi inayomkabili, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Chadema, Freeman Mbowe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Viongozi hao wamefikisha ombi hilo leo Jumatano, tarehe 2 Machi 2022, Ikulu jijini Dar es Salaam walipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Samia yaliyohusu masuala mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa na Zuhura Yunus, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu imesema, viongozi hao wa dini mbalimbali wamemwomba kutumia busara ili kuangalia namna kesi hiyo ya Mbowe na wenzake.
Mbali na Mbowe, wengine ni Halfan Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya ambao walikuwa makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam.
Washtakiwa hao wamekutwa na kesi ya kujibu na wataanza kujitetea Ijumaa hii, tarehe 4 Machi 2022 mbele ya Jaji Joachim Tiganga anayeisikiliza.
Aidha, viongozi hao wa dini wamezungumzia masuala ya elimu wakipendekeza kuwepo na mjadala mpana kuhusu mfumo mpya utakaokidhi mahitaji ya sasa kwa namna ya kutozilisha jamii ya wahitimu walioandaliwa kuajiriwa peke yake.
Vilevile, wameomba kutotozwa kodi ya mapato kwenye fedha ambazo zinapatikana kama misaada ya hiari ya wanachama na wafadhili kwa ajili ya kuendesha huduma zisizo za kibiashara zikiwemo huduma za wajane na yatima.
Yaani viongozi wote hawa wameshindwa kumpata hata mwanamama kiongozi mmoja wa kike kati yao? Ni dini gani hizi zinazowatenga wanawake katia uongozi?
Hawakuona aibu kukutana na Rais Samia na Zuhura Yunus?b
Madhehebu za Ahmadia na Bahai ziliwakilishwa?
Hongera Ben kwa kuliona hilo
Hao viongozi ni wadini kweli,maana nina mashaka na iman zao