Wednesday , 21 February 2024
Home Kitengo Maisha Afya Viongozi wa dini kutoa elimu ya ugonjwa wa Corona
AfyaHabari Mchanganyiko

Viongozi wa dini kutoa elimu ya ugonjwa wa Corona

Spread the love

MCHUNGAJI wa Kanisa la Makedonia Missions Centre-Kisasa Relini Jijini Dodoma, Chini ya Kanisa la Calvary Assemblies of God, Vicent Malendaa, amewataka watanzania kutofanya mzaha katika kutimiza masharti  ya serikali juu ya kujikinga na virusi vya ugonjwa wa Corona. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mchungaji  Malendaa akizungumza na waumini wa Kanisa hilo katika ibada maalum ya kuliombea taifa juu ya ugonjwa huo alisema kuwa kila mtanzania ni lazima kutumia taadhari ya kujikinga na virusi vya ugonjwa tishio wa kidunia unaotokana na virusi vya Corona.

Alisema kuwa ugonjwa huo ni tishio zaidi kwa dunia hivyo kila mmoja anatakiwa kuchukua tahadhari kwa kufuata maagizo ya serikali pamoja na wataalamu wa afya ili kuweza kukidhi malengo ya kujikinga na gonjwa hilo hatari.

Alisema kuwa pamoja na makanisa kufanya maombi ya kuliombea taifa ili Mungu aweze kulinusuru na ugonjwa huo, lakini kila mtanzania anatakiwa kufuata taratibu zote zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa vitakatisha mikono kwa lengo la kukabiliana na tatizo hilo.

Mbali na kufanya maombi kanisani hapo, Mchungaji Malendaa ameanzisha vipindi mbalimbali vya kutoa elimu kwa waumini wake juu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Coroma na kuhakikisha kila muumini anayeingia kanisani hapo anazingatia misingi, kanuni na sheria za kiafya zinavyoelekeza.

Mchungaji huyo alisema kuwa ameamua kuanzisha vipindi vya kutoa elimu kwa waumini wake kabla ya mahubiri ili kuweza kuwajengea misingi ya kujikinga na ugonjwa huo na kuwaonesha waumini kuwa Corona siyo ugonjwa wa kawaida.

Alisema hakuna sababu ya mtu yoyote kubeza au kukaidi kanuni za kujikinga na ugonjwa huo kwani kitendo cha kukaidi ni sawa na kosa la uhaini na mtu huyo anatakiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa maana hana mapenzi mema na taifa lake.

Katika hatua nyingine Mchungaji wa Kanisa la EAGT Kisasa C-Centre, Christian Katamba, amewakemea baadhi ya wanasiasa ambao wanageuza ugonjwa wa unaotokana na virusi vya Corona kuwa sehemu ya siasa.

Mchungaji Katamba alisema ugonjwa wa Corona ni ugonjwa mbaya ambao hautakiwi kufanyiwa mzaa wala kuchanganywa na siasa na ijulikane wazi kuwa kila mmoja anatakiwa kuchukua hatua za haraka na mathubuti katika kujikinga na ugonjwa huo.

“Nipende kusema kuwa hakuna nayeweza kukwepa ugonjwa huu na hakuna sababu yoyote ya kiongozi wa kisiasa kuchukulia ugonjwa huu kama sehemu ya kufanya siasa ila kinachotakiwa katika hili ni kuwa wamoja kwa kushirikiana kuhakikisha mapambano ya Corona yanafanyika” alisema Mchungaji Katamba.

Katika hatua nyingine Mchungaji Katamba alisema kuwa Kanisa la mahali pamoja kwa sasa limeanzisha maombi ya wiki nzima kwa lengo la kuliombea taifa na kumwomba Mungu ili aweze kuondosha jamga hilo la ugonjwa wa Corona.

Askofu wa Kanisa la EAGT Kanda ya Kati na mchungaji wa Kanisa la Mahali pamoja la Ihumwa, Robert Mangwelaa, alisema kuwepo kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona ni matukio ya kihistoria kutoka katika vitabu vitakatifu vya kibiblia ambapo kulishawahi kutokea ugonjwa ambao uliitwa Town.

Alisema kuwa ugonjwa huo uliua watu wengi sana katika mataifa mbalimbali lakini uliweza kutoweka kutokana na mshikamano wa viongozi mbalimbali wa kiimani kumwomba Mungu kwa nguvu na nia moja bila kuwepo kwa mgawanyiko.

Alisema kuwa hata hili linalotokea kwa sasa linaweza kuisha mara tu viongozi wote wa kiimani, kisiasa na kiserikali kama wataweza kushikamana na kunuia jambo moja kwa lengo la kumlilia Mungu na kufuata misingi inayotakiwa katika kujikinga na Corona jambo hilo linaweza kuisha.

Alisema kuwa magonjwa hatari kama hayo mara zote huwa ayabagui rangi, umri, utajiri, umasikini, elimu, asiyekuwa na elimu, wala dini bali ushambulia mtu yoyote ambaye anaweza kupatwa na janja hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakazi kwa mawaziri walia majitaka kusambaa mitaani

Spread the loveWAKAZI zaidi ya 4,000 wa mitaa ya Eyasi, TPDC na...

Habari Mchanganyiko

Viumbepori, bahari hatarini kutoweka

Spread the loveKUKOSEKANA juhudi za pamoja za Serikali, wadau wa uhifadhi na...

BiasharaHabari Mchanganyiko

TPSF yataja mbinu ya kuibua vipaji vipya taaluma ya madini

Spread the loveMkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Raphael Maganga...

Habari Mchanganyiko

Kampuni 500 kushiriki maonyesho ya TIMEXPO 2024

Spread the loveSHIRIKISHO la Wenye Viwanda nchini  ( CTI) kwa kushirikiana na...

error: Content is protected !!