VIONGOZI waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamewasili kituo cha Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa mahojiano kama walivyotakiwa na jeshi hilo jana. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).
Viongozi wa Chadema wanaotakiwa kuhojiwa ni Freeman Mbowe, John Mnyika, Salum Mwalim, Ester Matiko, Ester Bulaya, Dk. Vincent Mashinji na Halima Mdee.
Polisi wamewataka viongozi hao kuhoajiwa kuhusiana na kupigwa risasi kwa Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwelina Akwilini katika maandamano ya wafuasi wa Chadema yaliyofanyika Februari 16, mwaka huu, maeneo ya Mkwajuni jijini Dar es Salaam.
Mbali na viongozi hao lakini polisi wanawashikilia wanachama 42 wa Chadema pamoja na polisi sita kwa ajili ya tukio hilo na uchunguzi unaendelea.
Leave a comment