August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Viongozi wa Chadema washikiliwa polisi

Dkt. Vincent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema

Spread the love

DKT. Vincent Mashinji, Katibu  Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil Mwambe ambaye pia ni Mkiti wa Chama Kanda ya Kusini pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Zubeda Sakuru wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Mbamba Bay, anaandika Mwandishi wetu.

Taarifa kutoka ndani ya chama zinaeleza kuwa viongozi hao wamepelekwa kituoni kuhojiwa ambapo Katibu Mkuu Dkt. Mashinji ametakiwa kueleza kwanini yuko Mbamba Bay na aeleze amekwenda kufanya nini.

Polisi wamemkamata Katibu Mkuu Dkt. Mashinji, Mbunge Mwambe na Mbunge Zubeda baada ya kuvamia kikao cha ndani kilichokuwa kikiendelea mjini hapo ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu Dkt. Mashinji kukagua shughuli za chama katika majimbo ya kanda hiyo iliyoanza leo.

 

error: Content is protected !!