May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Viongozi TLS wanolewa kuzikabili kesi za kikatiba, haki za binadamu

Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa

Spread the love

 

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umefanya warsha ya kuwajengea uwezo viongozi wa kanda wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), katika kushughulikia kesi za kikatiba na haki za binadamu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Semina hiyo ya siku mbili kuanzia tarehe 20 hadi 21 Mei 2021, imefanyika jijini Dodoma, ambapo viongozi walioshiriki walipewa mbinu ya kutumia fursa na taratibu za kimahakama katika kutetea kesi hizo.

Akizungumza katika warsha hiyo, Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa amesema lengo lake ni kuwakumbusha viongozi hao, juu ya majukumu yao katika kusimamia kesi zinazohusu maslahi ya umma.

“Tumeona tuanze na hawa viongozi sababu wakurdi kwenye kanda zao, wanaweza kuweka mikakati na mafunzo endelevu kwa wanachama wao na kusimamia mawakili wao kufungua kesi katika kanda zao zinazohusu maslahi ya umma” amesema Olengurumwa.

Olengurumwa amesema“hii ni njia pekee tunadhani inakuwa ya kirahisi, sababu hii kazi ni sehemu yao, sio kazi mpya. Tunakwenda kuwakumbusha na kuwajengea uwezo kwenye kazi, kuendesha mashauri ya haki za binadamu haitofautiani na uendeshaji wa mashauri mengine.”

Kiongozi huyo wa THRDC amesema anaamini warsha hiyo itaongeza msukumo wa mawakili katika kuzifungua kesi mpya za kikatiba na haki za binadamu, pamoja na kusimamia kesi za aina hiyo zilizofunguliwa katika mahakama mbalimbali nchini.

“Iitakuwa ni jambo jema kama watabeba hiyo ajenda, wakirudi kwenye kanda zao wakashawishi wenzao angalau kwa mwaka wakawa na kesi mbili zinazohusu masilahi ya umma,” amesema Olengurumwa.

Olengurumwa amesema THRDC iliamua kuandaa warsha hiyo, kufuatia changamoto ya mawakili wengi kukwepa kusimamia kesi hizo, kwa madai kuwa hazina maslahi hasa malipo.

“Kumekuwa na uelewe mdogo wa wale mawakili kuhusiana na kesi za kimkakati, tumesahau kesi za haki za binadamau na katiba. Wengi wamejikita zaidi kwenye mashauri yenye maslahi binafsi, mfano ya kibiashara, kugombana mtu na mtu ukiachana na hizi za maslahi ya umma,” amesema Olengurumwa na kuongeza:

“Changamoto iliyopo wengi wanaamini ukiwa wakili katika masuala ya haki za binadamu, kikatiba na yenye maslahi ya umma unaweza ukawa masikini, hakuna malipo hakuna fedha.”

error: Content is protected !!