October 22, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yakiri kusababisha migogoro ya ardhi

Spread the love

SERIKALI imekiri kuwa viongozi wengi wa serikali za vijiji ndio chanzo cha migogoro ya ardhi nchini, anaandika Dany Tibason … (endelea).

Selemani Jafo, naibu waziri wa nchi ofisi ya rais, anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), ametoa kauli hiyo leo Bunegni Dodoma, wakati akijibu swali la nyongeza la Vedasto Ngombale, Mbunge wa Kilwa Kaskazini, wa Chama cha Wananchi (CUF).

Hata hivyo, serikali imesisitiza kuwa itachukua hatua kali dhidi ya viongozi wa aina hiyo, hasa wanaokiuka sheria na kusababisha migogoro kwa kuendekeza rushwa.

Mbunge huyo alitaka kujua sababu ya kukithiri kwa migogoro ya wakulima na wafugaji katika maeneo mengi nchini.

Alitaka kujua serikali inatoa wito gani kwa wafugaji wanaoruhusu mifugo yao kusaabisha hasara na njaa kwa wakulima.

Aidha, alitaka kujua serikali imejipangaje kuhakikisha mifugo haisababishi uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali na kuepusha uvunjifu wa amani.

Akijibu maswali hayo, Jafo amesema migogoro hiyo husababishwa na baadhi ya watendaji wa vijiji kutotambua umuhimu wa matumizi bora ya ardhi.

Jafo amesema kutokana na tatizo la mgogoro wa wakulima na wafugaji kuwa mkubwa kati ya wakulima na wafugaji, ameagiza wakuu wa wilaya na mikoa katika maeneo yote ya migogoro wawe na ajenda ya kudumu katika kuitatua.

error: Content is protected !!