Monday , 22 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Viongozi Serikali ya mitaa watakiwa kushirikiana na wananchi
Habari za Siasa

Viongozi Serikali ya mitaa watakiwa kushirikiana na wananchi

Mbunge wa Bahi, Omary Badwel
Spread the love

MBUNGE wa Bahi, Omary Badwel (CCM) amewataka viongozi wa serikali za mitaa kujenga tabia ya kuwashirikisha wananchi wao pale wanapohitaji kuanzisha miradi mipya. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo aliitoa katika mkutano wa hadhara wa usuruhishi kati ya Kampuni ya Mawasiliano ya simu za Mkononi ya TIGO na Yoramu Makapi kutokana na kutofautiana juu ya ujenzi wa kisima cha maji katika eneo lake.

Kutokana na hali hiyo Badwel alilazimika kuweka kambi katika kitongoji cha Zamahero, kijiji cha Mayamaya kwa siku nzima ikiwa ni juhudi za kutatua mgogoro uliojitokeza kati ya kampuni hiyo na mmiliki wa shamba ambaye ni Yoram Makapi.

Kampuni ya Mawasiliano ya TIGO ni miongoni mwa kampuni iliyojenga mnara wa mawasiliano iliyopo katika kijiji cha Mayamaya kitongoji cha Zamahero na kama ilivyo kawaida ya kampuni hiyo kuwapatia miradi mingine ya maendeleo wananchi wa eneo husika waliamua kuchimba kisima kirefu cha Maji katika kitongoji cha Zamahero ili kurahisisha huduma ya Maji katika kitongoji hicho.

Hata hivyo kazi ya kuchimba kisima ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika tarehe 9 Februari, mwaka huu familia ya mzee Yoram ambao ndiyo wenye eneo lililokuwa linachimbwa Kisima wakazuwia Uchimbwaji wa Kisima katika eneo lao.

“Kutokana na hali hiyo mmoja wapo wa wasimamizi katika kampuni hiyo alinipigia simu na kunielezea hali ilivyo na kueleza kuwa sasa kampuni itasitisha uchimbaji wa kisima hicho.

“Akanieleza kuwa kutokana na hali hiyo wanahamisha mradi wa uchimbaji wa kisima kwani hakuna maelewano, nilichokifanya mimi niliwaambia wasihamishe mradi huo na nitafika hapo ili tuweze kuzungumza na kuona tunafanyaje na niweze kujua tatizo liko wapi,” alieleza Badwel.

Katika mkutano huo mbunge alitaka kujua nini tatizo la kukwamisha mradi huo wa uchimbaji wa kisima kirefu cha maji.

Akieleza sababu ya kuwepo kwa kukwamisha mradi huo Mwenyekiti wa kijiji cha Mayamaya, Juma Chibalangu, alisema kuwa wafadhiri walifika hapo usiku wakataka wafanye survey ili wachimbe maji na kwa sababu walifika usiku na wao kueleza kuwa walikuwa na haraka ya kuchimba kisima ili waondoke ikabidi mwenyekiti, vyeo, na baadhi ya wajumbe wa serikali za kijiji wawapeleka wafadhili hao kwenye shamba la mmoja wa wananchi wa Mkondai ambae analima mashamba yake yaliyopo Zamahero kijiji cha Mayamaya.

Mwenyekiti alisema kuwa hata hivyo mmiliki wa shamba hilo hakuwa na taarifa  kuwa shamba lake litatumiwa kwa ajili ya kuchimba kisima cha maji.

“Baada ya mmiliki wa shamba kupewa tarifa alijitokeza na kuzuia licha ya kuambiwa kuwa kwa sasa hatua za maandalizi ya uchimbaji wa kisima umeishafikia asilimia 80 na uchimbaji utafanyika katika sehemu ndogo ya shamba lake,” alieleza Chibalangu.

Akizungumzia jambo hilo Badwel alisema kuwa pamoja na kwamba wafadhili wamefanya jambo jema la kuanzisha mradi wa uchimbaji wa kisima lakini yapo mapungufu kutoka katika serikali za mtaa husika.

“Yapo mapungufu yamefanywa na viongozi wa kijiji na ndo maana tumekwama na hapa hatuwezi kuendelea kuchimba kama wenye eneo lake hawajakubali kutoa eneo hilo hivyo Sasa hivi ni saa 6:17 mchana nahairisha huu mkutano hadi 9:00 alasiri ili mimi, Mbunge wenu pamoja na viongozi wa kijiji twendeni Mkondai kwa Mzee Yoramu ili tueze kuzungumza naye tufikie mwafaka na kwa kuwa mvua imenyesha na tupo viongozi wengi hivyo wote tutatumia pikipiki (bodaboda) hadi mkondai na saa 9:00 alasiri tukutane wote kwenye mkutano ili tupeane taarifa zilizo kamili,” alitoa agizo hilo Badwel.

Jitihada za kumtafuta mzee Yoramu ambaye ni mmiliki wa shamba hilo ziliweza kuzaa matuma kwani baada ya kuzungumza naye kwa mapana alikiri kutoshirikishwa na kutikujua nini faida ambaye angeipata wala kulipwa fidia.

“Mapungufu yaliobainika kujitokeza na kusababisha mzee Yoramu kukataa ni Viongozi wa kijiji walichukua eneo la Mzee  Yoramu  bila kumpa taarifa zozote ikiwa  eneo hilo ni shamba na mazao yapo.

“Hakupewa maelezo ya kina pale alipofika kwa viongozi kujua hatima ya eneo lake na mazao yake ambayo yameharibiwa na magari ya kuchimba visima.

“Wafadhiri kufika usiku na kuwataka viongozi wa kijiji wawatafutie eneo wapime, wachimbe waondoke haikuwa sawa kuwaharakisha hivyo viongozi wa kijiji,” alieleza Mzee Yoram.

Kutokana na hali hiyo pande zote zilikubaliana mambo yafuatayo. “Mzee Yoramu  ambae ndiye mmiliki halali wa eneo lake ambalo pia amelima kwa trekta na kuna mazao atapewa milioni moja, mzee huyo  atawaachia kijiji eneo hilo ili kazi ya kuchimba kisima iendelee.

“Viongozi wa kijiji wawe wanawashirikisha vizuri wananchi kabla ya kufanya maamuzi yalekuwa maazimio ya pande zote.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

Habari za Siasa

Makamba ataja maeneo ya kuboresha mambo ya nje

Spread the love  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika...

error: Content is protected !!