July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Viongozi Dumila wakamatwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Leonard Paul

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Leonard Paul

Spread the love

MAFTAHA Hamisi- Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tawi la Mbigiri Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro, ni miongoni mwa viongozi waliokamatwa na polisi kituo cha Dumila katika mazingira ya kutatanisha. Anaandika Bryceson Mathias, Kilosa … (endelea).

Katibu wa Tawi hilo, Mohamed Ami, ameliambia MwanaHALISIOnline kuwa Hamisi alikamatwa akiwa mjini Dumila na kwamba kabla yake, polisi walimkamata Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, Hemed Salum (CCM).

Amesema “Hamisi amekamatwa akiwa matembezini Dumila, pia na wengine waliokamatwa naye ni Mtendaji wa Mbigiri, Jacb Mvungi, ambapo makosa yao bado hayajawekwa wazi”.

“…siku moja kabla ya kukamatwa kwake, wafugaji wa jamii ya Kimasai waliingiza ng’ombe wao kwenye mashamba ya wakulima katika Kijiji cha Mbigiri, lakini wakulima hao walipoziswaga ili kuzipeleka polisi, kibao kiliwageukia”.

Mkuu wa polisi kituo cha Dumila (OCD), Jafari Kiyoga, alipoulizwa juu ya tukio hilo, alikataa kusema lolote akidai si msemaji ila Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Leonard Paul, ambaya hakupatikana kwa simu.

error: Content is protected !!