Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Viongozi DCPC wavuliwa madaraka, wachaguliwa wapya
Habari Mchanganyiko

Viongozi DCPC wavuliwa madaraka, wachaguliwa wapya

Spread the love

MKUTANO Mkuu Maalum wa Chama cha Waandishi wa Habari Dar es Salaam (DCPC) nchini Tanzania, umewavua nyadhifa viongozi wake kwa kutotimiza ipasavyo wajibu wao na kisha ukafanya uchaguzi wa viongozi wapya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkutano huo umefanyika leo Jumatatu tarehe 9 Mei 2022 na kuratibiwa na Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

Viongozi watano na wajumbe wa kamati ya utendaji wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Dar es Salaam (DCPC) wamevuliwa nyadhifa zao kwa kushindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo.

Waliovuliwa uongozi ni, Irene Mark (Mwenyekiti), Chalila Kibuda (M/mwenyekiti, Hussein Syovelwa (Katibu Mkuu), Fatuma Jalala (Katibu Msaidizi) na Patricia Kimelemeta aliyekuwa mweka hazina.

Wajumbe waliovuliwa ni Cecilia Jeremiah, Selemani Msuya, Kamugisha Mchunguzi na Christina Galaluhanga.

Hata hivyo, katika mkutano mkuu huo ulioitishwa na wanachama wenyewe, ulihudhuriwa na baadhi ya viongozi akiwemo Makamu Mwenyekiti, Chalila Kibuda, Naibu Katibu Mkuu, Fatuma Jalala, Mweka Hazina, Patricia Kimelemeta na wajumbe Shaban Matutu na Taus Mbowe.

Kabla ya wajumbe kuanza kujadili mwenendo wa DCPC, Taus Mbowe na Shaban Matutu walitangaza kujiuzulu.

Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan amesema, wameamua kuhudhuria mkutano huo kwani wao kama walezi wana wajibu wa kujua kinachoendelea na katika siku za hivi karibuni DCPC imekuwa nyuma kwa kila kitu.

“Kati ya Press Club zote Tanzania, DCPC ndiyo ya mwisho. Hii ndiyo imetufanya kufika hapa kujua kuna nini na tunawezaje kwenda mbele. Lengo letu DCPC iwe kubwa na kinara kwa Press Club zote Tanzania na hili linawezekana,” alisema Karsan

Mara baada ya majadiliano kuhusu uongozi uliokuwapo, mwanachama mmoja Ibrahim Yamola alitoa pendekezo lililoungwa mkono na wanachama la kuwavua uongozi waliosalia. Hata hivyo, baadhi yao waliovuliwa wakiwa ukumbini walichaguliwa tena kwenye nafasi mbalimbali.

Baada ya hatua hiyo, uchaguzi ulifanyika ambapo nafasi ya Mwenyekiti wa DCPC amechaguliwa Samson Kamalamo, Makamu Mwenyekiti Salome Gregory, Katibu Mkuu Fatuma Jalala, Katibu Mkuu Msaidizi Chalila Kibuda na mhazini Kimelemeta.

Wajumbe wapya waliochaguliwa ni Ibrahim Yamola, Salehe Mohamed, Tausi Mbowe, Janet Josiah, Shabani Matutu na Njumai Ng’ota.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo, Rais wa UTPC), Deo Nsokolo amesema wao wapo tayari kufanyakazi na uongozi uliochaguliwa huku akitoa wito kwa viongozi hao kuwatumikia wanachama bila ubaguzi wala upendeleo.

“Nina kufahamu vizuri Kamalamo, watumikie vizuri, uwe na ngozi ngumu na hakikisha unawaunganisha wote. Lakini kubwa nendeni mkaongeze wanachama, Dar es Salaam ina waandishi wengi, nendeni mkawaongeze,” amesema Nsokolo

Naye Kamalamo amewashukuru wanachama kwa kumuamini na kuahidi kwenda kuwatumikia huku akiomba ushirikiano wa kila mmoja, “sisi viongozi peke yetu hatuwezi. Tunaomba ushauri na michango yetu ya hali na mali.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB yakabidhi vifaa tiba hospitali Mtwara  

Spread the loveBENKI ya NMB Kanda ya Kusini imetoa msaada wa vifaa...

Habari Mchanganyiko

Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 

Spread the love  MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

error: Content is protected !!