September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Viongozi Bavicha watikisa mahakamani

Spread the love

BAADA ya viongozi wa kitaifa wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kusota rumande kwa saa 96 hatimaye leo wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka, anaandika Dany Tibason.

Watuhumiwa waliopandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma ni Mwenyekiti wa BAVICHA taifa, Patrobas Katambi,

Katibu wa BAVICHA, Julius Mwita, Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mbeya, George Tito na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji BAVICHA taifa, Joseph Kasambala.

Akisoma mashtaka yao mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Karayemaha na Wakili wa serikali, Lina Magoma alidai kuwa washtakiwa hao

wanashtakiwa kwa kukutwa na maandishi ya uchochezi kinyume na kifungu cha 32 (2) cha Sheria ya Magazeti sura namba 229 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Lina alidai kuwa washtakiwa watatu ambao ni Katambi, Mwita na Tito, mnamo Julai 8 mwaka huu walikutwa katika baa ya Captown mjini hapa wakiwa

na fulana zilizoandikwa lugha ya uchochozi.

Wakili wa serikali Lina alinukuu maneno hayo yaliyoandikwa katika fulana hizo kuwa yalikuwa yakisomeka “ Mwalimu

Nyerere: Demokrasia inanyongwa na Dikteta Uchwara”.

Hata hivyo alimsihi hakimu kuwa upelelezi wa kesi hiyo unaendelea na hakuna pingamizi na dhamana inaweza kutolewa kama watoa dhamana watakidhi masariti.

Katika washitakiwa hao Kasambala alifunguliwa jalada lake pekee ambapo shtaka lake linafana na wenzie isipokuwa mahali alipokamatiwa na ujumbe

kwenye fulana aliyokuwa ameivaa.

Kwa mujibu wa Wakili wa Serikali Beatrice Nsana, ameeeleza mahakama kwamba Kasambala Julai 9 mwaka huu alikutwa katika kituo cha Polisi cha kati akiwa amevaa fulana yenye maandishi “Mwalimu Nyerere: Demokrasia inanyongwa”.

Washtakiwa wote walikana mashtaka yao ambapo Hakimu Mfawidhi Karayemaha, aliwapa dhamana baada ya kutimiza masharti.

Hata hivyo kesi hiyo imeharishwa na itatajwa tena Julai 26 mwaka huu huku hakiwataadhalisha kutofanya kosa lolote kama hilo na wakifanya watafutiwa dhamana.

NJE YA MAHAKAMA

MUDA mfupi baada ya kupewa dhamana Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Taifa Patrobas Katambi,alisema msimamo wa vijana wa kudai haki hauwezi kusitishwa na mtu yoyote kwa kutoa vitisho.

Amesema anatoa ujumbe kwa rais John Magufuli kwa kumtaka akubali kukosolewa pale anapokosea na asichukie kuambiwa ukweli.

Mbali na hilo amesema ajitokeze kwa umma na kueleza kwamba mambo ambayo yanafanywa na jeshi la polisi kwa ajili ya kuminya demokrasia kwa vitendo vinavyotumiwa na jeshi la polisi kama ni agizo lake au la.

Amesema mara kadhaa siku ambazo wamekaa ndani kwa zaidi ya saa 96 walikuwa hawaambiwi kosa lao na walikuwa kwakidai kwamba wanatekeleza maagizo kutoka juu.

“Sina imani kama Rais Magufuli anatambua ukandamizwaji wa demokrasia ambao unaendelea kufanywa na jeshi la polisi dhidi ya wapinzani na kama hajui ni vyema ajitokeze adharani alieleza taifa kama ni maagizo yake au la na kama siyo maagizo yake IGP anatakiwa kujiuzuru” alisema Katambi.

Kuhusu IGP amesema anatakiwa kijiuzuru nafasi yake kutokana na kulitumia vibaya jeshi la polisi kwa ajili ya kukandamiza Demokrasia na kuendeleza uonevu ambao kimsingi ni sehemu ya kukatili.

Hata hivyo Katambi amesema kamwe vijana hawatanyamaza na wataendelea kutafuta haki zao na kuitetea Demokrasia kwa misingi ya kulinda katiba ambayo inaonesha wazi kuwa watawala wanaogopa kukosolewa.

“Sisi tulipokamatwa ilitumika nguvu kubwa zaidi kiasi kwamba sisi tulionekana kama waharifu hapakuwepo kwa mazungumzo yoyote kati yetu na jeshi la polisi matokeo yake tulipigwa na kupelekwa katika sero tofauti.

“Tulikuwa tukipelekwa katika sero tofauti tofauti na tulikuwa tukihamishwa bila hata kutoa taarifa kwa ndugu zetu wala kwa viongozi wenzetu jambo ambalo lilionesha wazi kuwa jeshi la polisi linakandaniza demokrasia na kuendeleza uonevu wa hali ya juu” amesema Katambi.

Kuhusu jinsi ya kuwepo kwa tamko la vijana kufika mjini Dodoma kushirikana na jeshi la polisi kwa lengo la kuzuhia mkutano wa CCM alisema BAVICHA wanaeshimu tamko la kiongozi wa Kitaifa Freemani Mbowe lakini watakaa na viongozi hao ili kujua sababu gani za kutofika Dodoma kwa lengo la kutimiza kile ambacho wamekiadhimia kwa kufika mjini Dodoma.

Hata hivyo alisema watafanya mkutano mkuu wa BAVICHA wa dharula ili kuona kama kuna uwezekano wa kufika Dodoma kwani watafanya kila mbinu kuhakikisha wanatafuta haki.

“Tunajua vijana tuko imara na lazima tutetee katiba ya nchi kwa kudai demokrasia ambayo watawala wanaonekana kuiminya haki tutaipata hapa duniani na tusipoipata duniani hakika tutaipata mbinguni” alisema Katambi.

Kwa uande wake wakili wa watuhumiwa hao Fredy Kalonga, alisema wateja wake wamepata dhamana na wanaenda kutipia hati ya mashitaka ili waweze kuendelea na mashitaka.

Amesema wateja wake ni watuhumiwa kwa hiyo bado makosa hayajajulikana na wataendelea kwa hoja ili kuhakikisha haki inatendeka.

Kesi hiyo ina mawakili watatu wakujitegemea ambaye ni Fredy Kalonga,John Chigongo na wakili wa kujitegemea ambaye amefahamika kwa jina moja la Mwaipopo.

error: Content is protected !!