January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Viongozi ADC watimka wajiunga UKAWA

Spread the love

VIONGOZI wa Chama cha Alliance for Democrat (ADC) mkoa wa Dodoma wamejiengua katika uongozi huo kwa madai chama hicho hakina nia ya dhati ya kufanya mageuzi kwa manufaa ya Umma. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Mbali na chama hicho kutokuwa na nia ya ukombozi uongozi wa juu kwa maana mwenyekiti wa ADC ambaye pia ni Mgombea Urais visiwani Zanzibar, Hamad Rashid kuwataka wanachama wa chama hicho kuunga mkono mgombea urais kupitia CCM.

Hayo yalielezwa jana na aliyekuwa mgombea udiwani kata ya Ipagala kupitia chama hicho Nyemo Mbijili, kubwaga manyanga na kujiunga na chama cha wananchi (CUF).

Mbiliji akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kampeni ya mgombea udiwani kata ya Ipagala, Dismas Thadei(CUF) uliofanyika katika viwanja vya stendi ya Majengo Mapya amesema ameamua kuondoka katika chama hicho kutokana na kutokuwa na nia ya dhati ya kufanya mabadiliko.

“Mimi nilikuwa mgombea udiwani wa kata ya Ipagala kupitia ADC lakini nimeamua kujiengua katika chama hicho na kuunga mkono mgombea wa CUF ambaye ni Damas Thadei,” amesema Mbiliji.

Mgombea huyo amesema kwamba yeye kama mgombea udiwani pamoja na viongozi wa mkoa katika chama hicho wamelazimika kuachia ngazi.

Katika kujiengua huko kulihusisha Mwenyekiti wa ADC mkoa wa Dodoma Mande Ndomondo ambaye naye alitangaza kujiondoa katika uongozi yeye pamoja na viongozi wengine.

Ndomondo amesema ADC ni chama ambacho hakiwezi kupeleka ukombozi kwa wananchi wanyonge nchini.

“Tumekuwa viongozi wa ADC lakini cha kushangaza viongozi wa juu wanaonekana kuwa tofauti na makubaliano mbali zaidi ni pale ambapo uongozi wa juu wanatuambia tuweke nguvu zaidi kwa udiwani na ubunge ila ngazi ya urais tuwachague CCM.

“Kwa hali hiyo na maagizo hayo kamwe hatuwezi kuendelea na chama ambacho hakina dila ya kuwakomboa watanzania wanyonge na masikini,” amesema Ndomondo.

Kwa upande wake mgombea udiwani kata ya Ipagala, Damas Thadei (CUF) amewataka wananchi kumchagua ili apambane na changamoto ya migogoro ya viwanja pamoja na ubovu wa miundombinu.

Amesema wakazi wa kata ya Ipagala wameendelea kuwa masikini kutokana na madiwani wote wa CCM waliopita kutojali masilahi ya watanzania.

error: Content is protected !!