April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Viongozi ACT-Wazalendo mbaroni kwa kufungua matawi bila kibali

Ado Shaibu, Katibu Mkuu ACT-Wazalendo

Spread the love

ADO Shaibu, Katibu wa Itikadi na Uenezi   wa Chama cha ACT Wazalendo, na viongozi wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufungua matawi bila kibali. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 14 Septemba 2019 na Salim  Bimani, Mwenyekiti wa Kamati ya Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma ACT-Wazaleno.

Kwa mujibu wa taarifa ya Bimani, viongozi hao wamekamatwa leo wakati wanafungua matawi mapya ya ACT-Wazaleno kwenye Kata ya Azimio, Jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, Ado pamoja na Soud Salum, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam, Risasi Semasaba Katibu wa Uchaguzi wa mkoa huo na Katibu wa Ngome ya Vijana wa Kata ya Azimio, Said wamepelekwa katika Kituo cha Polisi Chang’ombe.

“Polisi wanadai kushikiliwa kwa viongozi hao ni kukosa kibali cha ufunguaji wa matawi hayo. Viongozi hao wamepelekwa kituo cha Polisi Chang’ombe kwa mahojiano.

Chama cha ACT Wazalendo tunalaani kitendo hicho cha Jeshi la Polisi kuingilia masuala ya vyama vya Siasa na kuvizuia kutekeleza wajibu wao wa kisheria,” inaeleza taarifa ya Bimani.

Bimani ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kuwaacha huru wanasiasa hao sambamba na kusimamia wajibu kwa kukwepa kuvikandamiza vyama vya siasa vya upinzani.

error: Content is protected !!