Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Viongozi 150 kuchukuliwa hatua
Habari za Siasa

Viongozi 150 kuchukuliwa hatua

Spread the love

 

TAKRIBANI viongozi 150 hatarini kuchukuliwa hatua kali kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Viongozi hao wanadaiwa kushindwa kurejesha fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni ndani ya muda. Urejeshaji huo ulifika tamati Machi 2021.

Tuhuma zinazowakabili viongozi hao ni, kuchelewa kurejesha fomu hizo, kutotaja thamani ya mali, kutotamka baadhi ya rasilimali wanazomiliki na maslahi binafsi.

Viongozi 129 wanadaiwa kuchelewa kurejesha fomu hizo, huku 21 wakikutwa na mapungufu katika fomu zao walizozirejesha.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa, akizungumza bungeni jijini Dodoma, leo Alhamisi tarehe 22 Aprili 2021.

Waziri huyo wa utumishi amesema, viongozi 129 kati ya 15,110, hawajarejesha fomu hizo hadi mchakato huo ulipomalizika Machi mwaka huu.

Mchengerwa amesema viongozi 129 wametumiwa barua za kujieleza kwa nini wamechelewa kurejesha tamko hilo, na kwamba ikibainika hawakuwa na sabbau za msingi za kuchelewa, watachukuliwa hatua.

“Jumla ya Viongozi 129 sawa na asilimia moja ya Viongozi wote bado hawajarejesha tamko. Kwa mujibu wa Sheria ya Maadili Fungu 15 (c), kuchelewa kutoa tamko bila sababu za msingi ni kosa na ni ukiukwaji wa maadili.

Viongozi wasiorejesha wameandikiwa barua za kutoa maelezo na itakapobainika kuwa hawakuwa na sababu za msingi watachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa mbele ya Baraza la Maadili,” amesema Mchengerwa.

Mchengerwa amesema asilimia 4.1 ya viongozi 534 (viongozi 21) kati ya 609 waliohakikiwa , walikutwa na mapungufu kwenye matamko waliyotoa.

“Taarifa kuhusu zoezi husika inaonesha kuwa viongozi wa Umma 534 walihakikiwa sawa na asilimia 87.8. kati ya hao, matokeo ya uhakiki yanaonesha kuwa, asilimia 4.1 ya Viongozi waliohakikiwa kuna mapungufu kwenye matamko walioyatoa,” amesema Mchengerwa.

Mchengerwa amesema“Mapungufu hayo yanajumuisha, baadhi ya vipengele vya tamko kutojazwa kwa ukamilifu, kutotaja thamani ya mali, kutotamka baadhi ya rasilimali wanazozimiliki na kutotamka maslahi binafsi.”

Aidha, Mchengerwa amesema asilimia 2.4 ya viongozi hao wamebainika kuwa na viashiria vya Mmgongano wa Maslahi.

“Viongozi wote waliobainika na mapungufu, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma,” amesema Mchengerwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!