Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Vilio vyatawala wabunge wakimuaga Dk. Magufuli
Habari MchanganyikoTangulizi

Vilio vyatawala wabunge wakimuaga Dk. Magufuli

Spread the love

 

VILIO vimetawala viwanja vya Bunge jijini Dodoma, wakati wabunge wakiaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli (61). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Shughuli ya kuaga mwili wa Dk. Magufuli imefanyika leo asubuhi Jumatatu tarehe 22 Machi 2021, katika viwanja vya Bunge na kuongozwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Jeneza lenye mwili wa Dk. Magufuli, limewasili majira ya saa 2 asubuhi ukitokea Ikulu ya Chamwino, ulipolala tangu jana baada ya kuwasili kutoka Dar es Salaam.

Mara baada msafara wenye mwili wa Dk. Magufuli ulipowasili viwanja vya Bunge, vilio vilitanda kutoka kwa wabunge mbalimbali hali ambayo ilimfanya Spika Ndugai, kuwatuliza wabunge.

Akiwa mzungumzaji wa kwanza kwenye shughuli hiyo, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amesema, hana maneno mengi ya kumzungumzia, lakini kila mmoja anatambua safari yake ya kisiasa, ilifunguliwa na Dk. Magufuli.

Dk. Tulia ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini amesema, katika maisha yake hapa duniani, Dk. Magufuli ametenda mema licha ya baadhi ya watu kutoyaona.

Amesema, katika uchaguzi mkuu uliopita, wananchi walimchagua kwa kura nyingi Dk. Magufuli na mgombea wake mwenza, Samia Suluhu Hassan na kwa maana hiyo “sisi tunamwamini Mama Samia naamini kabisa kuwa atatufikisha.”

Naye Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Zubeir Ali Maulid amesema, “huu ni ushahidi kuwa Dk. Magufuli alikuwa mtu wa watu. Katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wake, kila mmoja ameona alichokifanya.”

“Katika kila anapopita wananchi wanajitokeza kusherekea maisha yake, ndivyo vile vile walivyokuwa wanajitokeza kipindi cha ziara zake. Huu ni ushahidi jinsi alivyokuwa anagusa maisha ya watu,” amesema Maulid.

“Tunamwomba Mungu amjaalie maisha mema na Watanzania tuendelee kumwombea kwani sisi sote tuko safarini kuelekea huko na Magufuli alikuwa ni binadamu, yawezekana alikwanza, tunaomba wamsamehe,” amesema.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema, binafsi inanipa shida kusema mbele yake, naona kama ananipa maelekezo, ananipigia simu “kwa kweli ananipa shida sana.”

Majaliwa amesema “kila mmoja ananamna ya kumwelezea, hata wananchi wameonyesha hilo, tumeona Dar es Salaam kwa siku mbili, tumeona Dodoma jana, kikubwa tumwombee.”

“Huzuni hii si yetu sisi tu, ni maeneo mbalimbali ya Afrika na nje ya Afrika kuwa alikuwa kiongozi wa watu. Leo tumepata fursa ya kuja kumuaga, kwa uzoefu nilioupata Dar es Salaam, wabunge msingeweza kumuaga na ndiyo maana tumeamua kumleta hapa,” amesema Majaliwa.

Majaliwa amesema, kutokana na umati huo, ndiyo maana “tumeamua kubadilisha utaratibu wa kumuaga. Hatuwezi kupita kimwona lakini tutampitisha maeneo mbalimbali.”

“Leo tupo hapa tunamuaga lakini mama yake yuko kitandani, tumwombee mama yake ilia pate nguvu,” amesema

Spika Ndugai amesema, “kwa miaka 26, Dk. Magufuli alipita katika lango hili au lile la Pius Msekwa kuingia bungeni tangu mwaka 1995 alipoingia kwa mara ya kwanza, aliingia kama mbunge, waziri na baadaye Rais. Leo tunamuaga kwa utumishi uliotukuka.”

Shughuli hiyo imehudhuliwa pia na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama akiwemo, Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo ambao wameweka mashada ya maua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mchina wa SGR aburuzwa kortini kwa kumjeruhi Mtanzania, TRC waja juu

Spread the love  RAIA wa China, Zheng Yuan Feng, amefikishwa mahakamani kwa...

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

error: Content is protected !!