Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Vilio, simanzi vyatawala miili askari ikiagwa Dar
Habari MchanganyikoTangulizi

Vilio, simanzi vyatawala miili askari ikiagwa Dar

Spread the love

 

VILIO na simanzi vimetawala wakati miili ya askari polisi watatu na mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA, ikiagwa katika viwanja vya Hospitali ya Polisi, Kurasini mkoani Dar es Salaam. Anaripoti Mwanaharusi Abdallah, TUDARCo … (endelea).

Tukio hilo lilitokea leo Ijumaa, tarehe 27 Agosti 2021, baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene na Inspekta Jenerali wa Polisi nchini, IGP Simon Sirro, kuwaongoza mamia ya waombolezaji kuaga miili hiyo.

Baada ya ndugu, jamaa na marafiki kuruhusiwa kuiaga miili hiyo, walianza kuangua vilio huku baadhi yao wakiishiwa nguvu na kupatiwa msaada na watu wao wa karibu.

Askari Polisi waliouawa kwa kupigwa risasi Jumatano tarehe 25 Agosti 2021, maeneo ya Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Kinondoni mkoani Dar es Salaam, ni Miraji Khatib Tsingay, Emmanuel Keralya na Kangae Jackson.

Mlinzi aliyefariki ni Joseph Okotya Mpondo.

Shangazi wa marehemu Jackson, Unisia Benjamin, amesema alipokea msiba wa ndugu yake kwa masikitiko makubwa.

“Nilipokea taarifa ya msiba wa Jackson kwa uchungu sana, niliumia sana sababu ni mtoto wa kaka yangu, ameniuma sana. Jack alikuwa mtoto mzuri mwenye hekima, heshima na msaada wangu nimeumia sana,” amesema Unisia.

Baada ya miili hiyo kuagwa, ilipakizwa katika magari kwa ajili ya kupelekwa katika familia zao kwa taratibu za mazishi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!