Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Vijiji vyote kufikishiwa umeme Desemba 2022
Habari Mchanganyiko

Vijiji vyote kufikishiwa umeme Desemba 2022

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imesisitiza ifikapo Desemba 2022, vijiji vyote vya Tanzania Bara, vitakuwa vimefikishiwa umeme na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Anaripoti Jemima Samwel DMC … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Steven Byabato, wakati akijibu swali la mbunge wa Bukoba Vijijini, Jasson Rwaikiza.

“Je, ni lini umeme utapelekwa katika Vijiji vya Buzi, Buguruka, Musina, Nsheshe na vingine ambavyo havijafikiwa na umeme katika Jimbo la Bukoba Vijijini,” amehoji Rweikiza

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Byabato amesema, Serikali kupitia REA, inaendelea kupeleka umeme na kufikisha katika vijiji vyote vya Tanzania Bara ifikapo Desemba, 2022.

“Vijiji vinane kati ya vijiji 94 vya Bukoba Vijijini ambavyo ni Buzi, Buguruka, Musira, Nsheshe, Ngarama, Omubweya, Kagarama na Rukoma vinatarajiwa kupatiwa umeme kupitia mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili,” amesema Byabato

“Mradi huu ulianza kutekelezwa Machi, 2021 na unatarajia kukamilika Desemba, 2022. Gharama ya mradi ni Sh.2.04 bilioni,” amesema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!