July 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Vijana wavamia, wapora Dar

Spread the love

KUNDI la vijana wakiwa na mikuki, mapanga na magobole wamevamia nyumba kadhaa za wakazi wa Buza, Mjimpya jijini Dar es Salaam na kupora vitu mbalimbali vya thamani usiku wa kuamkia leo, anaandika Hamisi Mguta.

Taarifa kutoka kwa baadhi ya waliokumbwa na mkasa huo zinaeleza kuwa, tukio limetokea usiku wa saa nane ambapo kundi hilo linalokadiriwa kuwa na vijana zaidi ya 20, lilipita nyumba hadi nyumba na kuvunja milango huku wakishinikiza kupewa pesa.

Mwandishi wa habari hizi amefika eneo la tukio na kushuhudia uharibifu uliofanywa na vijana hao ambapo Masaoud Ngoshani, aliyekumbwa na tukio hilo amesema, baada ya tukio hilo waliungana usiku kutoa taarifa katika kituo kidogo cha Buza.

“Tulipotoa taarifa katika kituo kidogo walituambia gari lao ni bovu hivyo wameshindwa kufika hadi tumeamua kuwapigia makao makuu ndio wakatupa taarifa kuwa wanakuja.

“Huu unatokana na uzembe wa polisi wetu, yaani hata kuja kuona namna tulivyoathiliwa ni shida,” amesema.

Hata hivyo, mwandishi wa habari hizi alishuhudia polisi kutoka kituo cha Chang’ombe walifika katika eneo la tukio mchana wa saa sita na nusu wakiwa na siraha za mabomu ya machozi.

Amesema, matukio haya yamekua yakijitokeza mara kwa mara na kwamba watuhumiwa hukamatwa na baadaye huachwa huru bila kushughulikiwa.

“Wamenichukulia simu tano na pesa zaidi ya milioni moja ambazo nyingine zilikua ni pesa za kazini nilizotakiwa kulipa mahala,” amesema Ngoshani.

Aisha Joseph, aliyekutwa na mkasa huo amesema, yeye na familia yake walipata taarifa kutoka kwa majirani zao ndipo walipokaa tayari kwa kujikinga nao.

Na kwamba, hawakufanikiwa kuwazuia kwani waliporwa simu lakini hawakufanikiwa kuchukuana Televisheni baada ya kuiangisha huku filimbi za polisi jamii zikiwa zinapulizwa.

“Yaani ni vijana wengi, hata jirani hawezi kutoa msaada wa haraka bila kuwepo kwa jeshi la polisi,” amesema Betty John, mmoja wa waathirika hao.

error: Content is protected !!