January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vijana watakiwa kutobaki nyuma

Spread the love

VIJANA wametakiwa kushiriki kikamilifu katika vyombo mbalimbali vya utoaji wa maamuzi na uchaguzi wa viongozi katika uchaguzi mkuu 2015. Anaandika Faki Sosi, DSJ … (endelea).

Hayo yamesemwa wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana iliyofanyika leo, Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Akitoa hotuba kwa vijana kuhusu ushiriki na ushirikishwaji, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Ole Gabriel amesema vijana wanahitaji kushiriki kutoa maamuzi mbalimbali ya uchaguzi.

Gabriel amesema serikali imefanikiwa kuongeza umri utakaotambulika kuwa ni kijana kutoka miaka 18 hadi 45 kufikia miaka 15 hadi 35, hivyo mtu yeyote mwenye umri kati ya miaka 15 na 35 anafaa kuitwa kijana na anaweza kushiriki katika maamuzi yanayomuhusu kijana ikiwemo kupiga kura.

Aidha ameeleza kuwa vijana wanatakiwa kuwa na tabia ya kujitolea katika jamii kwani vijana wana nafasi muhimu kwa jamii.

“Vijana sio tatizo bali vijana ni fulsa, kura ya kijana ndio itakayochagua Tanzania ijayo, pia ujana sio umri wa kudumu hivyo muutumie ujana wenu ili mkumbukwe,” amesema Gabriel.

Naye mmoja wa vijana waliohudhulia katika maadhimisho hayo, Irene Lyamuya amesema vijana ndio nguvu kazi ya Taifa hivyo wanahitaji kushirikishwa katika kuchagua viongozi mahili na kutoa maamuzi pia amewataka vijana kujitokeza katika kupiga kura na kutochagua viongozi ambao wanatoa rushwa.

Siku hiyo maalum ambayo yalianzishwa mwaka 1999, yakiadhimishwa kila tarehe 12 ya kila mwaka, Tanzania yalianza kuadhimisha mwaka 2000.

error: Content is protected !!