Thursday , 7 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Vijana washauriwa kukopa kukuza uchumi
Habari Mchanganyiko

Vijana washauriwa kukopa kukuza uchumi

Wajasiriamali
Spread the love

VIJANA waliohitimu elimu ya juu nchini wameshauriwa kuanzisha shughuli za ujasiriamali na kukuza uchumi wao kwa kujitokeza kwenye ofisi za mikopo badala ya kusubiri ajira ambazo kwa sasa bado ni kitendawili, anaandika Christina Haule.

Meneja wa kanda ya Morogoro wa Mfuko wa kujitegemea (PTF) Christopher Peter amesema hayo jana mara baada ya kusaini makubaliano na Taasisi isiyo ya kiserikali inayohusika na masuala ya kusaidia vijana na wanawake katika kuboresha shughuli za maendeleo ijulikanayo kama (Yes I Do) ili waweze kupata vijana wengi watakaopata mikopo na kujiendeleza kiuchumi na kutimiza lengo la Serikali la kukuza uchumi kwa jamii.

“hakuna sababu kwa sasa vijana kutembea na bahasha kila siku mikononi wakitafuta ajira, bahasha hadi inachanikia mkononi na wote hatuwezi kuajiriwa serikalini, fursa za kujiendeleza na kukuza uchumi wa kila mtu zipo sambamba elimu mliyoipata itumieni” amesema Peter.

Peter amesema kuwa wamekuwa wakishughulika na shughuli za utoaji mikopo lakini muitikio kwa vijana umekuwa mdogo tofauti na kinamama na makundi maalum licha ya mikopo wanayoitoa kuwa na riba nafuu ambapo mkopo wa mwezi mmoja unalipiwa riba ya 1% huku mkopo wa mwaka ukilipia riba ya 12% kwa makundi yote yakiwemo kimama, vijana, watu wenye ulemavu na wanaoishi na VVU.

“mfano mtu akikopa shilingi milioni moja kwa miezi sita atarudisha shilingi milioni 1,060,000 kwa maana ya riba ya shilingi 60,000 pekee”, amesema Peter.

Hivyo amesema, anaimani kupitia shirika hilo wanaweza kupata vijana wengi zaidi ambao wanaweza kuwakopesha huku nao (PTF) wakiendelea kuwahimiza vijana kujitokeza na kupata fursa hizo.

Rais wa Yes I do, Bahati Richardson amesema wanatarajia kuanza kusaidia makundi ya vijana na kinamama 804 wanaojishughulisha na kilimo huku wakiendelea kuwakusanya vijana wengine wa makundi ya biashara, viwanda vidogo vidogo na wabunifu wa teknolojia mbalimbali ili kuwajengea uwezo wa kukuza uchumi wao.

Richardson amesema anaimani kupitia PTF vijana wengi wataweza kuwafikia makundi yote wakiwemo vijana nchi nzima kuanzia kwenye wilaya, kata hadi vitongoji kwa kipindi chote cha makubaliano cha mwaka mmoja yaani kuanzia mwezi Aprili 2017/18.

Hata hivyo aliwaasa wanaotegemea kukopa na kwenda kulipa mikopo mahali pengine kuacha mara moja tabia hiyo kwani haitaweza kuonesha manufaa ya mkopo.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Shura ya Maimamu kukata rufaa kupinga Sheikh kufungwa miaka 7

Spread the loveSHURA ya Maimamu Tanzania, inakusudia kukata rufaa dhidi ya hukumu...

Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza...

Habari Mchanganyiko

NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang

Spread the loveWaathirika wa maporomoko ya tope Wilayani Hanang, mkoani Manyara, waliopoteza...

Habari Mchanganyiko

TPF-NET Arusha yaonya jamii ya wafugaji zinazoendeleza ukatili wa watoto na wanawake

Spread the love  MTANDAO wa Polisi wanawake wa Arusha kuelekea siku 12...

error: Content is protected !!