Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Vijana waruka ukuta wa Mirerani kuchimba Tanzanite’
Habari Mchanganyiko

Vijana waruka ukuta wa Mirerani kuchimba Tanzanite’

Spread the love

FATUMA Kikuyu, mchimbaji mdogo wa madini kutoka mgodi wa Tanzanite ulioko Mirerani mkoani Manyara amesema kuna baadhi ya vijana wanalazimika kuruka ukuta wa mgodi huo kwa ajili ya kufanya shughuli za uchimbaji, kutokana na kushindwa kukidhi masharti yaliyowekwa na serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kikuyu amesema hayo leo tarehe 22 Januari 2019 mbele ya Rais John Magufuli katika mkutano wa wadau wa sekta ya madini uliofanyika jijini Dar es Salaam, na kuiomba serikali kulegeza masharti ili vijana hao waingie kihalali mgodini humo kufanya uchimbaji kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.

Amesema tangu serikali ijenge ukuta huo na kuweka masharti kwamba kila mchimbaji anayetaka kuingia kwenye mgodi wa Tanzanite kuwa na mkataba wa ajira pamoja na mashahara, vijana wengi wamekwama kukidhi masharti hayo na kuishia nje.

“Vijana walioko migodini ni wa chache, vijana wengi wako nje hawawezi kuingia kwa sababu hawana mikataba na mishahara, ungetuachia geti wazi. Vijana wanajitahidi kuruka ukuta ili waingie wafanye kazi, wanajeshi wamesema wakikamata kijana anaruka ukuta atapata adhabu kali. Kazi ya Tanzanite inataka vijana wengi sababu kuipata ni sawa na umbali nguzo sita za umeme kuelekea chini.,” amesema Kikuyu.

Kikuyu ameeleza kuwa, wachimbaji wengi wanakabiliwa na ukosefu wa mitaji kitendo kinachopelekea kushindwa kuwalipa mishahara na kutoa mikataba kwa vijana hao, kitendo kinachopelekea kukosa sifa za kuingia katika mgodi huo.

“Geti la Magufuli tunaomba utuondolee masharti , mimi sina uwezo wa kulipa mshahara vijana. Migodi yote hakuna mtu anataka msaharaha wanataka ten percent (asilimia kumi), ile kazi inataka vijana wengi, wengi wako nje ya ukuta wa Magufuli, vijana wako wataruka ukuta wakiingia ndani watapigwa risasi, waache vijana wako wafanye kazi,” amesema Kikuyu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!