January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vijana waliponda Baraza waliloundiwa

Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Vijana Tanzania, Elly Ahimidiwe Imbya

Mratibu wa Baraza la Vijana Tanzania, Elly Ahimidiwe Imbya

Spread the love

SHIRIKA la Vijana la Restless Development Tanzania, wanatarajia kumwandikia Rais Jakaya Kikwete kumwomba asiusaini Muswada wa Sheria ya Baraza la Taifa la Vijana uliopitishwa na Bunge, kwa madai kwamba vijana hawakushirikishwa. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Shirika hili linatekeleza mradi wa ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika mchakato wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 nchini. Mradi huu ulianza mwaka 2013 na unatekelezwa katika mikoa 18 Tanzania.

Lengo ni kuwashirikisha vijana katika mchakato wa katiba mpya, kuwahamasisha katika swala la kugombea nafasi mbalimbali kwani vijana wengi hawatambui wajibu wao katika jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari leo nje ya mdahalo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Baraza la Vijana Tanzania, Elly Imbya, amesema vijana wengi hawakushirikishwa katika upitishwaji wa muswada huo na maoni yao yote yaliyopendekezwa yamekatwa na kuweka ya Seikali.   

Imbya amesema, “hii ilitokea tena mwaka 2013 ambapo vijana waliandaa muswada na kumpa Mbunge wa Ubungo, John Mnyika awasilishe bungeni, kama kijana mwenzetu, lakini umekataliwa na serikali ikidai ni muswada binafsi, kitu ambacho hakina ukweli.”

“Tunaomba serikali ipitie upya muswada huo, na itusikilize, hatuna haraka na katiba mpya, hivyo tutaifakari vizuri ili baadaye isije kuleta matatizo. Wakumbuke maamuzi ya leo ndo matokeo ya kesho,” amesema Imbya.

Aidha, Imbya ameishauri serikali kuwapa kipaumbele vijana kwani ndio nguvu kazi ya taifa na ndio viongozi wa kesho. Kwamba wasiangalie maoni ya vijana wa mjini tu bali hata wale wa vijijini, kwani wana mitazamo yao na wana haki ya kushiriki katika shughuli za vijana.

error: Content is protected !!