November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Vijana waitwa mapambano dhidi ya mimba za utotoni, UKIMWI

Mkurugenzi wa Taasisi ya Youth and Alive Initiative, Sesilia Shirima.

Spread the love

 

TAASISI ya Young and Alive Initiative (YAI), imeanza kusaka Vijana, kwa ajili ya programu maalumu ya kuwajengea uwezo watu wa rika hilo (YAI Champion Fellowship), kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo afya ya uzazi na ujasiriamali. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa jana Ijumaa, tarehe 5 Agosti 2021 na Mkurugenzi wa YAI, Sesilia Shirima, akiitambulisha programu hiyo  mkoani Dar es Salaam.

“Leo hii tuko mbele yenu kuwatanbulsiha programi yetu inaitwa YAI Chamoion Fellowship. Kama tulivyo wajuza taasisi yetu inaitwa Young and Alive lakini haimaanishi tutakuwa vijana milele, kwa hivyo lengo la mradi wetu ni kujenga uwezo kwa vijana kuanzia miaka 15 noaka 24 outambua na kuwa viongozi katika kufilisha taarifa za afya ya uzazi kwa vijana wenzao na huduma kwa kutumia nguzo tatu za uongozi kama utoaji huduma za uchechemuzi na ujasiriamali jamii,” amesema Shirima.

Shirima amesema mafunzo hayo yatakuwa ya mara kwa mara ambapo kila kundi litaoata mafun,o hayo kwa muda wa miezi nane.

“Tutakuwa tulishirkiana na wadau mbalimbali kufanya mafunzo haya, mfano utahusisha wadau wanaofanya uchechemuzi, ukasiriamali jamii na utoaji huduma ili waweze kutoa ujuzi wao kwa vijana,” amesema Shirima.

Amesema mpango huo unalenga kuunga moono jitihada za Serikali katika kuimarisha afya kwa makundi ya vijana balehe, ili kuounguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa vijana, mimba za utotoni na kuounguza ukatili wa kijinsia.

“Vipaumbele hivi vitatu vikubwa vyote vinalenga eneo la afya ya uzazi na hivyo jitihasi za kuhakikisha moango huu unatimia zinatuhitaji sisi vijana,” amesema Shirima.

Mkugenzi huyo wa YAI amewataka vijana wenye nia ya kuwa mabalozi wa afya hasa ya uzazi, kuomba nafasi za kushirli katika programu hiyo, kuanzia tarehe 8 Novemba hadi 5 Disemba 2021, na kwamba majina ya watakaochaguliwa yatatangazwa tarehe 20 Disemba mwala huu.

Naye Afisa Mradi wa YAI, Getrude Clement, amewataka vijana kushirki katika programu hiyo, ambayo itashirkisha vijana wa mikoa yote nchini.

error: Content is protected !!