Tuesday , 30 May 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Vijana wa kilimo Moshi waipigia chapuo CCM
Habari za Siasa

Vijana wa kilimo Moshi waipigia chapuo CCM

Spread the love

MUUNGANO wa Vijana wa Kilimo cha kitalu nyumba (MVIKIKINYU) katika halmashauri ya Moshi mkoani Kilimanjato, umeipongeza serikali kwa kuwapa elimu ya mkulima na kuwawezesha kumiliki kitalu nyumba kinachowasaidia kujiongezea kipato. Anaripoti Mwandishi Wetu, Moshi … (endelea).

Kutokana na hayo, wameahidi kuhakikisha wanakichagua tena Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kiendelee kuongoza na wao kama vijana waendelee kunufaika.

Wakizungumza na amsha amsha 2020 ya Uhuru FM wilayani humo, wamesema awali maisha yalikuwa ya shida kutokana na kukosa kufanya shughuli yoyote ya kuwaongezea kipato lakini kupitia asilimia 10 ya mapato inayotolewa na halmashauri kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu imewasaidia sana.

“Sisi kama vijana hapa kazi yetu kubwa ilikuwa kukaa vijiweni, hatukuwa na shughuli yoyote ya kufanya, wakati mwingine tunagombana na wazazi lakini ukiangalia ni vile wamechoka kutuhudumia maana tulikuwa mzigo kwao,  lakini kwa sasa tunamshukuru Mungu tunajihudumia wenyewe na kusaidia familia zetu,” alisema Katibu wa MVIKIKINYU, Frank Kimaro wa Uru Kusini.

Alisema kwa sasa jukumu lao kubwa ni kuhamasisha vijana wenzao ili katika uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020 kura zote ziende kwa CCM kwa kuwa ndicho chama kilichoonyesha dhamira ya dhati a kuwakumbatia vijana.

Kwa upande wake, Anthony Maro mkazi wa Uru Kusini alisema kupitia kitalu nyumba hicho jamii sasa inawaamini na fursa nyingi zimejitokeza katika sekta ya kilimo.

“Hapa mnapoona hii ni awamu ya pili, awamu ya kwanza tulilima tumepata faida na kupitia kilimo hicho tumepata mwamko na tunalima na kwingine,” alisema.

Aliwahimiza vijana wengine kujiunga kwenye vikundi ili serikali iweze kuwasaidia kwa kuwawezesha mikopo na ujuzi hivyo kuzalisha ajira na kujiongezea kipato.

Akitoa taarifa ya mradi huo, afisa maendeleo ya jamii wilaya, Restina Mwasha alisema halmashauri hiyo ni miongoni mwa halmashauri zilizopata fursa ya kujengewa kitalu nyumba kwa ajili ya kuwawezesha vijana kupata ujuzi na stadi za kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia ya Kitalu nyumba (Greenhouse technology) unaotekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu.

Alisema awamu ya kwanza ililenga vijana 20 na mafunzo yalitolewa mwaka 2019 na awamu ya pili ilifanyika 2020 lengo likiwa ni kuongeza tija na kuvutia vijana wengi kujiajiri katika kilimo.

Alitaja baadhi ya mafanikio ya mradi huo ni vijana kupata mafunzo ya kilimo ambapo walitambua fursa mbalimbali zilizopo na namna ya kuzitumia, vijana wameweza kujiongeza na kuumia fursa katika eneo hilo kwa kulima mboga za majani.

Aliweka bayana matarajio ya vijana wanaosimamia kitalu hicho kuwa ni kujenga vitalu kwenye maeneo yao kupitia uwezeshaji wa mikopo isiyo na riba kutoka halmashauri, kuanzisha kiwanda kidogo cha ukaushaji wa mazao ya mbogamboga na matunda na kuanzisha uchakataji wa vyakula vyote vya mifugo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari za Siasa

Musoma Vijijini waomba ujenzi wa barabara uanze haraka

Spread the loveJIMBO la Musoma Vijijini, mkoani Mara, limeomba Serikali kuhakikisha ujenzi...

Habari za Siasa

ACT Wazalendo yaanika madudu miradi ya ujenzi, moundombinu

Spread the loveCHAMA cha ACT Wazalendo kimeeleza wasiwasi juu ya uelekeo wa...

Habari za Siasa

Samia ashuhudia utiaji saini ujenzi wa minara 758 ya bilioni 265

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa kampuni za...

error: Content is protected !!