August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vijana wa Burundi ”wazamia” nchini Marekani

Pierre Nkurunziza, Rais wa Burundi

Spread the love

VIJANA sita wakiwamo wavulana wanne na wasichana wawili kutoka  Burundi waliokuwa wakishiriki katika mashindano ya roboti yaliyokuwa yakifanyika  jijini Washington DC, wametoweka nchini Marekani na haijulikani walipo hadi sasa,  anaandika Catherine Kayombo.

Waliotoweka nchini Marekani ni  Don Ingabire, Kevin Sambukiza,Nice Munezero, Audry Mwamikazi, Richard Irakoze na Aristide Irambona.

Waandaaji wa mashindano hayo ya kwanza duniani wamesema kuwa wametoa taarifa polisi baada ya msimamizi wa timu hiyo ya Burundi kushindwa kuwapata vijana hao.

Msemaji mkuu katika mashindani hayo, Jose Escotto amesema ripoti kuu imeshawasilishwa kwa polisi na wako wanachunguza kupotea kwa vijana hao.

Idara ya polisi jijini Washington, imesema kuwa vijana hao walionekana kwa mara ya mwisho siku ya jumanne wakati wa kufunga michezo hiyo.

Imebandika picha za vijana hao katika mtandao wa twitter na kuwataka raia kuwasiliana nao endapo watawaona vijana hao.

error: Content is protected !!