December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

‘Vijana tumieni mitandao kwa tija’

Given Edward akipokea tuzo kutoka kwa Malkia Elizabeth wa Uingereza

Spread the love

VIJANA nchini  wameshauriwa kujituma na kuwa wabunifu katika matumizi ya mitandao ya kijamii ili kuisaidia jamii badala ya kupoteza muda kwa kufanya mambo mabaya yasiyokuwa na tija. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Aidha, vijana wengi zaidi wa kitanzania hususani kwa maeneo mjini, muda mwingi hutumia mitandao kwa kufanya mambo mabaya yakiwemo ya wizi, utapeli na mengine badala ya kujifunza mazuri yanayofanywa na watumiaji wengine wa mitandaoni.

Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na vijana wawili Angela Benedicto na Given Edward, ambao walitunukiwa  tuzo za The queens young leader’s awards  na Malkia Elizabeth wa Uingereza, zilizofanyika katika makazi yake Buckingham place Jijini London.

Vijana hao wa kitanzania ambao walipata tuzo hizo wiki moja iliyopita, baada ya kazi zao  na michango mbalimbali ya kuisaidia jamii kwa kupitia mitandao kutambuliwa.

Watanzania  watanzania hao ni miongoni mwa vijana 60 wenye umri kati ya miaka 18-29 kutoka nchi mbalimbali waliojitokeza kuwania tuzo hizo.

Wakizungumza kwa furaha baada ya kurejea nchini, vijana hao wamesema, vijana bado wanafursa na nafasi ya kufanya makubwa katika jamii zao.

Akizungumza na waandishi leo mmoja kati ya vijana hao, Given Edward (21 ambae  ni Mkurugenzi na mwazilishi wa  mtandao wa MyElimu ambao unawezesha vijana  na wanafunzi wa shule za sekondari Tanzania kufanya mijadala inayohusu  masomo.

“Nilipitia changamoto nyingi katika masomo yangu ndipo nilipoona umuhimu na kuanzisha  mtandao huu ili kuwasaidia wanafunzi wengine ambao wanachangamoto kama zangu” amesema Edward.

Nae Angela Benedicto (28) Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Wote sawa la Jijini Mwanza linalofanya utetezi wa wafanyakazi wa majumbani na kutoa elimu kwa wazazi.

Benedicto amesema, “Chanzo cha wafanyakazi wadogo wa ndani ni wazazi wenyewe ambao wanaruhusu watoto wao kwenda kufanya kazi. Lakini pia, naisaidia jamii kwa kutoa elimu ya kuto wazarau wafanya kazi wa ndani kwani wote nisawa”.

Amesema  baada ya kupokea tuzo hizo wamesema, walipata fursa ya kutembelea sehemu mbalimbali iliwa ni pamoja na kupata mafunzo kutoka kwa viongozi wa nchini humo.

“Tunapenda kutoa wito kwa vijana wenzetu kuwa wabunifu na kujitolea katika kuisaidia jamii  kwa mafunzo tuliyoyapata na tuzo hii sio zetu peke yetu bali ni kwa ajili ya watanzania wote”amesema.

error: Content is protected !!