Friday , 9 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Vijana nyoronyoro waonywa
Habari Mchanganyiko

Vijana nyoronyoro waonywa

Spread the love

ASKOFU wa Kanisa la Asembless Of God,Mlima wa Moto Jimbo la Dodoma na Nyanda za Juu Kusini,Silvanus Komba amewataka vijana kufaya kazi kwa bidii na kuachana na tabia ya ulegevu na uzembe. Anaripoti Danson Kaijage… (endelea)

Askofu Komba alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na vijana wa kanisa hilo lililopo Sabasana Jijini hapa mud mfupi baada ya kumalizika ibada maalum ya kuwahamasisha waumini wa kanisa hilo na watanzania kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii badala ya kusubiri miujiza.

Kiongozi huyo wa Kiroho alisema kwamba ni aibu kuona kijana akifanya kazi kwa ulegevu, au kukaa vijiweni akipiga soga badala ya kufanya kazi kwa bidii na kwa wakati ili kujipatia naendeleo.

Kutokana na hali hiyo Askofu Komba alisema kuwa umefika wakati wa vijana kufanya kazi kwa bidii zaidi kuliko kipindi kingine chochote kwa maelezo kuwa hakuna mtu ambaye anaweza kupata maendeleo bila kufanya kazi.

Sasa nataka vijana wote wa kanisa hili kuhakikisha tunapanga siku ya kukutana hapa kanisani ili tuweze kupeana mbinu mbalimbali za kufanya kazi, sitaki kuona kijana ndani ya kanisa akifanya kazi kwa uzembe.

Hata kama ni dada wa kazi ni lazima ufanye kazi kwa bidii ili uweze kumshangaza mwajiri wako na ili uweze kufanikiwa ni lazima uhamke mapema na kufanya kazi, suala la ufanyaji kazi kwa bidii siyo mapenzi ya mtu bali ni maagizo kutoka kwa Mungu mwenyewe” alisema Askofu Komba.

Mbali na kuwataka waumini wa kanisa hilo kufanya kazi kwa bidii pia aliwaonya kutokuwa watu wa kuwategemea watu wengine kwa lengo la kupewa misaada badala yake wajifunze wao kutoa misaada kwa watu wengine ambao ni wahitaji.

Pamoja na kufanya kazi kwa bidii vijana wametakiwa kutenga muda wa kufanya mazoezi ya viungo ikiwa ni pamoja na kukimbia angalau kilomita saba ili kujenga afya zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!