July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vijana nchini watangaziwa neema

Vijana wakiosha magari kupata ujira

Spread the love

SERIKALI imesema jumla ya sh. Bilioni  5 zimetengwa kwa ajili ya kuwawezesha vijana nchini kukopa na kuanzisha shughuli za kujiajiri katika sekta mbalimbali. Anandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Hayo yamesemwa leo bungeni na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa (CCM).

Jumaa alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwawezesha vijana hao kwa kuwakopesha fedha na kuwapa elimu ya ujasiriamali ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Akijibu swali hilo, Kabaka amesema  serikali katika mwaka fedha 2015/16 kupitia utekelezaji wa Programu ya Ajira kwa vijana imetenga Sh. Bilioni 5 kwa ajili ya kuwawezesha vijana nchini.

Amesema  katika kufanikisha utekelezaji wa programu ya kukuza ajira kwa vijana, wizara hiyo Novemba, 2014 ilisaini makubaliano ya utekelezaji wa Programu hiyo na Wakuu wa mikoa yote nchini.

Aidha,amesema  makubaliano hayo yanabainisha wajibu wa majukumu ya mikoa na mamlaka za serikali za mitaa katika utekelezaji wa programu ya ajira kwa vijana pamoja na ukuzaji wa ajira katika ngazi husika.

“Naomba kutumia fursa hii kutoa wito kwa waheshimiwa wabunge wote ambao pia ni madiwani katika maeneo yao, serikali za mikoa pamoja mamlaka za serikali za mitaa kutekeleza makubaliano haya ipasavyo,”amesema Kabaka.

error: Content is protected !!