Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Vijana ACT-Wazalendo: Ukosefu ajira ni hatari zaidi ya UVIKO-19
Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo: Ukosefu ajira ni hatari zaidi ya UVIKO-19

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo, Mkoa wa Dar es Salaam, Felix Kamugisha
Spread the love

 

NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, Mkoa wa Dar es Salaam, kimeomba Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, itekeleze kikamilifu sera za nchi zinazolenga kumaliza tatizo la ukosefu wa ajira, kwa kuwa changamoto hiyo ni hatari zaidi ya ugonjwa wa Virusi vya UVIKO-19. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online, kwa njia ya simu leo tarehe 24 Februari 2023, Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo, Mkoa wa Dar es Salaam, Felix Kamugisha, amesema Serikali inapaswa kuchukua hatua za dharura kukabiliana na changamoto hiyo, kama ilivyopambana kutokomeza UVIKO-19.

“Tuna sera nzuri sana, tatizo letu ni kutafsiri sera tulizojiwekea kwenda kuwa kitu halisi, hapa ndipo panahitaji tafsiri sahihi ya kiongozi ni nani na anafanya nini kwa muda gani. Serikali inapaswa kuchukua tahadhari na kuongeza jitihada kumaliza tatizo hili,” amesema Kamugisha.

Ameongeza “Serikali ilitazame suala hili kama ilivyotazama UVIKO-19 ilipoingia nchini, kwa kuchukua hatua za dharura kukabiliana nalo, ndivyo pia iweke mikakati katika kuinua uchumi wa vijana kupitia ajira.”

Aidha, Kamugisha amewataka watendaji wa Serikali kuwa na desturi za kufuatilia vijana wasiokuwa na ajira katika maeneo yao, ili wajue madhila wanayokabiliana nayo.

“Kijana ninayemzungumzia mimi ni yule ambaye anaishi chini ya dola moja ya kimarekani, anaokota chupa anakusanya mzigo akauze kilo moja kwa Sh. 250, afikishe kilo ngapi apate kula? Huyu anahitaji kutazamwa kwa upekee sana. Serikali inawajibika kumfikia na kumtatulia changamoto zake na kumuwekea mazingira rafiki ya kujiajiri,” amesema Kamugisha.

Mwenyekiti huyo wa vijana ameishauri Serikali iwekeze katika kuboresha mazingira ya sekta ya sanaa na michezo nchini, kwa kuwa inaongoza kutoa ajira kwa vijana “kama tungeweza boresha sekta hii ya michezo na burudani ikawa kama sekta ya viwanda, vijana wangapi wangepata ajira?”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!