October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vigogo wawili wasakwa kwa ununuzi haramu wa dhahabu

Madini ya dhahabu

Spread the love

NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameagiza Jeshi la Polisi kuwakamata wafanyabiashara Mansoor Almasi na Jacob Mwapinga wanaotuhumiwa kufanya ununuzi haramu wa madini ya dhahabu kwenye Mgodi wa Ulata ulioko mkoani Iringa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Nyongo ametoa agizo hilo baada ya wafanyabaishara hao kukaidi wito wake pamoja na kuonana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.

Katika hatua nyingine, Nyongo ameagiza jeshi la polisi kuwakamata wamiliki wa mgodi wa dhahabu wa Nyakavangala, kufuatia wamiliki hao kuwasilisha kwake taarifa isiyo sahihi kuhusu namna ya mgodi huo unavyoendeshwa,  ulipaji kodi na mrabaha wa serikali.

Nyongo yuko ziarani mkoani Iringa, ambapo katika ziara yake alizungumza na wachimgaji wadogo na mmiliki wa mgodi wa Ulata, Ibrahimu Msigwa.

error: Content is protected !!