Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Vigogo wamiminika mkutano mkuu CCM, Profesa Lipumba na Mrema ndani
Habari za Siasa

Vigogo wamiminika mkutano mkuu CCM, Profesa Lipumba na Mrema ndani

Spread the love

MKUTANO Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania umeanza leo Jumamosi tarehe 11 Julai 2020 ukiwa na agenda mbalimbali ikiwemo kuwathibitisha wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Mkutano huo unafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa CCM wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma ambapo wageni mbalimbali wamehudhuria kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Miongoni mwa wageni ni viongozi wa vyama vya upinzani ambao ni wenyeviti, Profesa Ibrahim Lipumba (CUF- Chama cha Wananchi), Augustine Mrema, (Chama cha Tanzania Labour Party-TLP), John Cheo (DP) na Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa, John Shibuda.

Pia, wasanii mbalimbali wapo katika mkutano huo, miongoni ni; Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz, Ali Salehe Kiba (Ali Kiba), Mbwana Yusuph Kilungi (Mbosso), Mwanahawa Abdul Juma (Qeen Darlin), Shetta, Mwana FA.

Marais wastaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria mkutano huo.

Pia, mawaziri wakuu wastaafu wa Tanzania, Mizengo Pinda, Cleopa Msuya, Jaji mstaafu Joseph Warioba, Frederick Sumaye na John Malecela na Edward Lowassa.
Katika mkutano huo, amehudhuria aliyewahi kuwa katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Maspika wastaafu wa Bunge la Tanzania, Pius Msekwa na Anne Makinda. Pia, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amehudhuria.

Pia, waliokuwa wabunge, mameya na wenyeviti wa Halmashauri wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamehudhuria mkutano huo.

Baadhi ya agenda za mkutano huo utakaomalizika kesho Jumapili ni kuthibitisha wagombea wa Urais wa CCM, wa Tanzania na Zanzibar, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, walipitishwa jana tarehe 10 Julai 2020 katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).

Rais John Magufuli amepitishwa tena na wajumbe wa NEC kutetea kiti chake cha Urais wa Tanzania, huku Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ambaye pia ni Mtoto wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, alichaguliwa kugombea Urais wa Zanzibar.

Dk. Mwinyi aliteuliwa kwa kupata kura 129 sawa na asilimia 78.65, akiwashinda wenzake Shamsi Vuai Nahodha aliyepata kura 16 na Dk. Khalid Salum Muhamed aliyepata kura 19.
Katika kinyang’anyiro hicho Rais Magufuli alikuwa mtia nia wa pekee wa CCM katika kugombea Urais wa Tanzania.

Pia, katika mkutano huo, wagombea 32 waliojitosa katika mbio za Urais wa Zanzibar wamehudhuria mkutano huo ambapo Dk. Mwinyi aliibuka mshindi.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online kwa habari zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!