Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Vigogo wamiminika bungeni, JPM kulifunga Bunge
Habari za Siasa

Vigogo wamiminika bungeni, JPM kulifunga Bunge

Marais Wastaafu wa Tanzania
Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Magufuli leo Jumanne tarehe 16 Juni 2020 analihutubia Bunge la 11 na kulivunja jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea),

Bunge hilo la 11 linaloongozwa na Spika Job Ndugai lilizinduliwa na Rais Magufuli tarehe 20 Novemba 2015.

Tayari wageni mbalimbali wa Kitaifa na Kimataifa wamekwisha kuwasili ukumbini kumsubiri Rais Magufuli kuingia ndani ya ukumbi huo.

Baadhi ya wageni hao ni; Marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete.

Pia, Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar, Mohamed Ali Shein, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Ali Seif Iddi, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na Makamu wa Rais mstaafu wa Tanzania, Mohamed Gharib Bilal.

Kulifunga Bunge hilo, kunatoa fursa ya mchakato wa uchaguzi mkuuutakaofanyika Oktoba 2020 kuanza.

Wengine waliopo ni, mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye, Mizengo Pinda na Edward Lowassa.

Pia, Spika Mstaafu Anne Makinda, Jaji Mkuu mstaafu, Othuman Chande, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ni miongoni mwa waliojitokeza katika shughuli hiyo ya kihistoria.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI ONLINE & MwanaHALISI  TV kwa habari zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!