April 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Vigogo wa Chadema Songwe, watoka gerezani 

Spread the love

VIONGOZI kadhaa wandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika mkoa wa Songwe na jimbo la Tunduma, hatimaye wametoka gerezani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Songwe … (endelea).  

Taarifa zilizothibitishwa na mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka zinasema, viongozi hao waliachiwa leo Ijumaa, tarehe 27 Machi 2020, baada ya baada ya kusota mahabusu kwa takribani miezi mitano. 

Mwakajoka amewataja waliochiwa kwa dhamana, ni pamoja na mwenyekiti wa mkoa wa Songwe, Isakwisa Thobias Lupembe.

Wengine waliochiwa huru kwa dhamana, ni Mhazini wa jimbo la Tunduma, Hamza Hussen Mpongolela; Mwenyekiti wa jimbo hilo, Boniphace   William Mwakabanje na mlinzi (RB) wa jimbo hilo, Eliah Mwabukusi.

Washitakiwa wote kwa pamoja, wametuhumiwa na Jamhuri kwa kosa la “kusudio la mauwaji dhidi ya Julius Mwavelenga,”na kufikishwa mahakamani mwishoni mwa mwaka jana.

Mwavalenga aliwahi kuwa mwanachama na diwani wa Chadema katika kata ya Sogea, jimboni Tunduma.

Alitangaza kukihama Chadema miaka mitatu iliyopita na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kile kinachoitwa, “kufika bei.”

error: Content is protected !!